Kongamano la jinsia lafanyika chuo cha DIT Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini wametakiwa kuzingatia masomo katika kozi walizochagua kusoma badala ya kuweweseka na mahusiano ya kimapenzi kabla ya wakati.
Rais hiyo imetolewa Novemba 16, 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za watoto na wanawake la KIVULINI, Yassin Ally wakati akiwasilisha mada kwenye kongamano la kuwajengea uwezo wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliochaguliwa kujiunga na Chuo cha DIT Kampasi ya Mwanza.
Katika kongamano hilo, wanafunzi wametahadharishwa kuepuka viashiria vya matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ikiwemo ubakaji na ulawiti ambayo yamekuwa yakiripotiwa katika vyombo vya habari yakiwasibu baadhi ya wanafunzi.
Nao baadhi ya wanafunzi walioshiriki konamano hilo, wameeleza kuwa litawasaidia kupata uelewa wa maisha ya chuo na kujiepusha na marafiki wenye vishawishi visivyofaa.
Mkuu wa Chuo cha DIT kampasi ya Mwanza, Dkt. Albert Mmari amesema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kufundishia chuoni.
Chuo cha Teknolojia Dar es salaam (DIT) kampasi ya Mwanza kupitia dawati la jinsia chuoni hapo kimekuwa kikiandaa makongamano mbalimbali ili kuwajengea uwezo wanafunzi kujiepusha na matukio ya ukatili wa kijinsia na badala yake kuzingatia masomo yao.
Mkuu wa Chuo cha DIT kampasi ya Mwanza, Dkt. Albert Mmari akifungua kongamano hilo.
Mkuu wa Chuo cha DIT kampasi ya Mwanza, Dkt. Albert Mmari akifungua kongamano hilo.
Mkuu wa Chuo cha DIT kampasi ya Mwanza, Dkt. Albert Mmari akifungua kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.

Wanafunzi wa DIT Mwanza wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.
Wanafunzi wa DIT Mwanza wakifuatilia kongamano hilo.
Wanafunzi wakifuatilia mada.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: