LIVE STREAM ADS

Header Ads

Zoezi la uokoaji laendelea vyema Kariakoo Dar

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais Dkt.Samia aagiza ukaguzi maghorofa yote.

Wakati zoezi la uokoaji likiendelea katika ghorofa lililoanguka Kariakoo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezitaka mamlaka zinazohusika kuchukua hatuna stahiki ikiwemo ya kuyafanyia ukaguzi majengo ya ghorofa yaliyojengwa na yanayoendelea kujengwa ili kubaini uimara wake.

Dkt. Samia ametoa maagizo hayo katika taarifa yake kwa umma kuhusiana na ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salam hivi karibuni.

Alieleza kuwa hatuna hiyo itasaidia kubaini ubora wa majengo hayo na kuepusha madhara kwa watu na mbali zao.

Aidha alilitaka jeshi la polisi kumuhoji mmiliki wa jengo hilo ili kusaidia uchunguzi na kupata ukweli juu ya sababu za kuporomoka kwa jengo hilo.

Aidha Dkt. Samia amempongeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na vyombo vya ulinzi, wadau mbali mbali na wananchi kwa kushiriki katika uokoaji na kuahidi serikali kugharamia matibabu pamoja na mazishi ya watu waliopoteza maisha.

Pia Dkt. Samia ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa watu waliofariki katika mkasa huo na kuwatakia ahueni ya haraka manusura wa tukio hilo ambao hadi Jumapili Novemba 17 jumla ya watu 13 walithibitishwa kufariki dunia.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.