LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la KIVULINI laendesha kongamano la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la kutetea haki za watoto na wanawake la KIVULINI, limeendelea kuhamasisha wananchi wenye sifa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongozi na Vijijini unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Akizungumza Jumapili Novemba 17, 2024 kwenye kongamano lililowakutanisha waendesha bodaboda, bajaji, mawakala wa mabasi pamoja na abiria katika stendi ya Nyamhongolo Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Mkurugenzi wa shirika hilo, Yassin Ally amesisitiza shughuli za kiuchumi zisiwanyime wananchi haki yao ya kupiga kura.

Nao baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wameeleza utayari wao wa kujitokeza kupiga kura huku Mwenyekiti wa Bodaboda Kituo cha Nyamhongolo, Charles Budeba akitangaza kutoa ofa maalumu siku ya uchaguzi.

Naye Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Nyamhongolo, Mecktrida Lyimo ambaye pia ni Afisa Mtendaji wa Kata hiyo, amesema suala la ulinzi na usalama litaimarishwa ili wananchi wapige kura kwa amani.

Hili ni kongamano la tatu kuandaliwa na shirika la KIVULINI ambapo kongamano la kwanza lilijumuisha viongozi wa dini mkoa Mwanza huku kongamano la pili likiwakutanisha wakilishi wa makundi ya kijamii wakiwemo vijana na wanawake wilayani Magu.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally.
Mwenyekiti wa Bodaboda Kanda ya Nyamhongolo, Charles Budeba akizungumza kwenye kongamano hilo.
Naye Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Nyamhongolo, Mecktrida Lyimo ambaye pia ni Afisa Mtendaji wa Kata hiyo akizungumza kwenye kongamano hilo.
Bodaboda akichangia hoja kwenye kongamano hilo.
Mwananchi akichangia mada kwenye kongamano hilo.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia kongamano la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji 2024 lililofanyika Nyamhongolo wilayani Ilemela.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.