Rais Samia akamilisha miradi 354 ya maji
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Miradi hiyo ambayo inasimamiwa na Serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu imesaidia kupeleka huduma bora za maji katika maeneo ambayo awali yalikosa huduma ya uhakika ya maji.
Aidha serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Maji imeendelea kutekeleza miradi ya uhifadhi wa vyanzo vya maji ambapo takribani miradi 104 ya uhifadhi na uendelezaji wa vyanzo vya maji imetekelezwa.
Serikali itaendelea kusimamia miundombinu ya maji ili kuzuia upotevu pamoja na wizi wa maji ili kuwezesha huduma hizo kuwafikia wananchi kwa ufanisi zaidi.
#KaziInaongea
No comments: