LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia atoa Millioni 100 Kijiji cha Nyasaungu, Musoma

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Tujiandae kushiriki ipasavyo kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji Novemba 27, 2024.

Afya ni mtaji hivyo ndivyo unavyoweza kusema na ukweli wa hilo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaujua na ndio maana ameridhia serikali yake kutoa kiasi cha Tsh 100 milioni kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Nyasaungu, kilichopo katika jimbo la Musoma vijijini mkoani Mara.

Kijiji cha Nyasaungu kina vitongoji vitano na kwa sasa kinakamilisha ujenzi wa zahanati hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutoa huduma za Afya Disemba 01, 2024

Nyasaungu ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Ifulifu kikiwa pamoja na kijiji cha Kabegi na Kiemba ambavyo kila kimoja kina Zahanati yake.

Kukamilika kwa Zahanati hiyo kutavifanya vijiji vya Kata ya Ifulifu kila kimoja kuwa na zahanati yake.

Mbali na fedha kutoka serikalini, lakini pia wananchi kwa umoja wao wamechangia fedha na nguvu kazi kwa kushirikiana na mbunge wao Profesa Sospeter Muhongo.

Jengo kuu la Zahanati hiyo liko katika hatua za mwisho kabisa za kukamilika, choo chenye matundu matatu kinajengwa na muda wa ujenzi unapaswa kuisha Novemba 30, 2024.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.