Mwanza wajipanga kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wakazi wa Jiji la Mwanza wamesema wako tayari kujitokeza kwenye kampeni za uchaguzi wa Serikali za Miaa, zinazotarajiwa kuanza Novemba 20, 2024 ili kusikiliza sera za wagombea kwa ajili ya kufanya maamuzi sahihi wakati wa kupiga kura Novemba 27, 2024.
Wakizungumza Jumanne Novemba 19, 2024 kwenye mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi uliofanyika Kata ya Luchelele, wamesema wanatarajia kuona wagombea wakinadi sera na si vinginevyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akitoa hamasa kwa wananchi kushiriki ipasavyo uchaguzi huo, amewakumbusha wagombea kufuata sheria ili kuwa na kampeni pamoja na uchaguzi wa amani.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: