DC Nyamagana akemea kampeni chafu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi ametoa rai kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kunadi sera zao wakati wa kampeni ili kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani.
Makilagi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Wilaya ya Nyamagana ametoa rai hiyo Jumatatu Novemba 18, 2024 wakati akitoa elimu na hamasa kwa wananchi katika Kata ya Mahina kuhusu umuhimu wa kushiriki uchaguzi huo.
Katika hatua nyingine Makilagi amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hivyo ni vyema wananchi wakatumia haki yao ya kujitokeza kupiga kura kuwachagua viongozi bora watakaoshirikiana pamoja kwenye shughuli za maendelo katika mitaa yao.
Mwananchi akichangia hoja kwenye mkutano huo.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI
No comments: