LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali, wadau kusaidia watoto wenye maradhi ya moyo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeweka mkakati wa upatikanaji wa taarifa na huduma za afya kwa watoto wenye maradhi ya moyo ili kupunguza changamoto ya gharama za matibabu kwa watoto wanaohudumiwa na Taasisi ya Moyo ya JKCI.

Tatizo la moyo kwa watoto limeonekana kuongezeka ambapo kati ya watoto 100 wanaozaliwa mtoto mmoja anabainika kuwa na tatizo la moyo.

Katika jitihada hizo chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Benki ya NMB imeingia makubaliano ya ushirikiano wa miaka minne na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 1 ambayo itatolewa kwa awamu nne kusaidia matibabu ya watoto wenye maradhi ya moyo wanaopata huduma katika taasisi hiyo.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge na kushuhudiwa na Afisa Mkuu wa Fedha JKCI, Agnes Kuhenga ambapo utekelezaji wa makubaliano hayo unatarajiwa kuanza rasmi mwaka huu.

Lengo la makubaliano hayo ni kuwezesha upatikanaji wa taarifa na huduma za afya kwa watoto wenye maradhi ya moyo na kupunguza changamoto ya gharama za matibabu kwa watoto wanaohudumiwa na Taasisi hiyo ikiwa ni sehemu ya sera ya NMB kuwekeza kwenye Jamii.

Mbali na mchango wa kifedha, ushirikiano huo umelenga kushirikiana na Wataalamu wa JKCI kutoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa wafanyakazi wa benki hiyo, wateja na wadau wengine ili kuongeza uelewa kuhusu afya ya moyo miongoni mwa Watanzania na kushiriki kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo.

Asilimia 70 ya gharama za matibabu kwa watoto huchangiwa na Serikali lakini pamoja na kuchangiwa, bado asilimia 80 hawamudu gharama hizo kwa asilimia 30 iliyobaki ambapo kiwango cha gharama kwa upasuaji kwa mtoto mmoja ni kati ya Shilingi milioni tano hadi milioni 15.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), taasisi hiyo inafanya upasuaji kwa watoto 357 kwa mwaka.

Kutokana harambee iliyowahi kufanywa na Taasisi ya Heart Foundation (HTAF), wanatarajia kuongeza upasuaji wa watoto kutoka idadi hiyo hadi watoto 500 kwa mwaka.

Kisenge amesema ushirikiano kati ya JKCI na HTAF ulianza mwaka 2023 kwa nia ya kusaidia watoto wenye magonjwa ya moyo na kuungana na serikali katika kusaidia matibabu ya watoto.

Watoto wengi wanapata tatizo la moyo kwa kuzaliwa nalo na katika watoto 100 mmoja ana tatizo la moyo, aidha inakadiriwa kwa wastani wa watoto Milioni mbili wanaozaliwa kwa mwaka nchini, 13,000 hadi 14,000 kati yao wana tatizo hilo na 4,000 watahitaji upasuaji wa moyo.

Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo na Bingwa wa Magonjwa ya Moyo JKCI, Dkt. Sulende Kubhoja naye anasema, ongezeko la idadi ya watu nchini, linakwenda sambamba na idadi ya watoto wanaozaliwa na matatizo ya moyo.

Mwaka 1962 Watanzania tulikuwa takribani Milioni 10 na sasa ni idadi imeongezeka na kufukia Milioni 61 ambapo asilimia 60 nchini ni watoto walio na umri wa miaka 16 na asilimia 80 ya Watanzania ni walio katika umri wa miaka 40 ambao wako kwenye umri wa kuzaa.

Kwa wastani watoto Milioni mbili huzaliwa kila mwaka na katika hawa, kuna watoto takribani 10,000 wanazaliwa na tatizo la moyo na wengine watahitaji upasuaji ambapo upasuaji mmoja unaweza kufika Shilingi Milioni 15 hadi 20.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.