Gharama za nishati kushuka zaidi Tanzania
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Mwaliko huo umetolewa Novemba 05, 2024, katika Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika nchini Afrika Kusini kupitia ofisi ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi ambayo imebainisha kuwa fursa zilizopo katika sekta hiyo ni vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia, miundombinu ya mafuta na gesi, miradi ya nishati jadidifu na viwanda vya petrokemikali.
Kwa upande wa vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia tayari Wizara ya Nishati imekamilisha maandalizi muhimu kuelekea tukio la uzinduzi wa duru ya tano ya kunadi vitalu vya mafuta na gesi asilia vilivyo wazi ambao utaanza rasmi Machi, 2025 wakati wa mkutano na Maonesho ya Petroli ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es Salaam.
Tanzania itanadi Jumla ya vitalu 26 vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini. Kati ya vitalu hivyo, vitalu 23 vipo eneo la baharini na vitatu vipo eneo la Ziwa Tanganyika.
Pamoja na vitalu hivyo, ipo fursa kwa wawekezaji kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuendeleza vitalu vya Eyasi-Wembere, Mnazi Bay Kaskazini na Songo Songo Magharibi; vitalu ambavyo TPDC imeendelea kuvifanyia utafiti wa mafuta na gesi asilia.
Aidha vitalu vyote vitakavyowekwa sokoni ni vile vinavyoendeshwa na TPDC kwa lengo la wawekezaji kuona na kushiriki mnada huo kikamilifu.
Maeneo mengine ya uwekezaji katika sekta ya gesi asilia ni uwekezaji katika ujenzi wa vituo vya kujaza gesi asilia kwenye magari na viwanda vya petrokemikali kwa kutumia gesi asilia.
Serikali ya Rais Samia imefanya kazi kubwa ya kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kutekeleza miradi ya kimkakati kama vile Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP), hivyo Tanzania ni sehemu sahihi kwa uwekezaji.
#KaziInaongea
No comments: