Rais Samia, shujaa wa maendeleo Tanzania
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema mafanikio yote yanayopatikana nchini yanatokana na ushupavu wa Kiongozi Mkuu wa Nchi, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameelezwa kuipokea nchi katika mazingira ambayo siyo ya kawaida na katika mapito magumu.
Ameeleza kuwa Tanzania kama nchi imepitia nyakati ngumu ambazo mara nyingi huyafanya mataifa kutetereka, hata hivyo maono na ushupavu wa Rais Samia umesababisha nchi kuwa salama na tulivu.
"Sio nchi nyingi hizi changa kama ya kwetu ambazo zinaondokewa na Kiongozi Mkuu wa nchi katikati ya safari bila kutarajia zikabaki salama, hata ukayasahau yote lakini kumbuka tuna Taifa ambalo bado ni salama, lina umoja na amani kwa sababu tuna Kiongozi Mkuu aliye shupavu hilo ni jambo la msingi" ameeleza Profesa Kitila.
#KaziInaongea
No comments: