TAKUKURU yatoa tahadhari Uchaguzi Mdogo
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan haitaki kabisa kuona vitendo vya rushwa vinafanyika kwa namna yeyote ile itakayochochea kumfanya mtu ashinde kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.
Hitaji la Rais Samia ni kuona kunakuwa na uchaguzi wa huru na haki bila kujali ni mgombea wa chama gani atashinda.
Kwa kulifanikisha hilo Novemba 26,2024, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Ilala imesema itachuka hatua kwa yeyote atayepokea, kutoa au kujihusisha na rushwa.
Hayo ameyasema Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala Sosthness Kibwengo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam.
"Uchaguzi ni maisha uchaguzi ni maendeleo tunaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa tufahamu kwamba rushwa ni kikwazo katika maendeleo, rushwa ni kikwazo kufanya uchaguzi ambao upo sahihi, rushwa ni kikwazo katika kukuwezesha wewe katika kuchagua kiongozi ambaye ni bora"
"Katika kuwakumbusha wananchi tumefanya vipindi 41 vya redio, tumefanya zaidi ya mikutano 69 ya hadhara, tumefanya semina 33 kwa makundi mbalimbali ikiwamo semina ya viongozi wetu wa dini ambao tuliwaomba walisemee jambo hilo kwenye nyumba za dini na kuwataka watu wajue umuhimu wa kuzingatia maadili katika suala la uchaguzi" amesema Kibwengo
Aidha Kibwengo amesema uchaguzi huu ni muhimu hivyo wananchi wajitokeze na wachague viongozi sahihi kwa maendeleo ya nchi.
#KaziInaongea
No comments: