LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yapunguza vifo vya wajawazito

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Ni haki kwa kila mama mjamzito anayejifungua kuishi, ndio maana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Uongozi wa Rais Dt. Samia Suluhu Hassan, inafanya jitihada za hali na mali kuhakikisha vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua vinapungua kwa kiasi kikubwa.

Katika kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Samia, umeweza kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua kwa asilimia 81 na hii imetokana na Matunda ya Uwekezaji sahihi katika kuboresha Sekta ya Afya.

Takwimu za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa, vifo vya wajawazito kwa mwaka 2016 vilikuwa 556 ambapo hadi kufikia mwaka 2023 vifo hivyo vimepungua na kufikia 104 kwa kila vizazi 100.

Miongoni mwa sababu zinazotajwa kuchangiwa kupungua kwa vifo hivyo ni pamoja na mtindo wa maisha wenye afya unaozingatia lishe bora, mazoezi na kuepuka vitu vinavyoweza kuwa na madhara kwa mjamzito ili ujauzito uendelee kukuwa vizuri.

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO nchini Tanzania, baada ya kushuhudia ongezeko la vifo vya wajawazito waliweka mikakati ya pamoja kuhakikisha vifo hivyo vinatoweka kabisa.

Kutokana na wajawazito kupata ugumu wa kuvifikia vituo vya afya, WHO ilitafuta fedha ya kusaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu na kuongeza maarifa kwa wataalamu wa afya ambapo Serikali iliboresha miundombinu katika hospitali mbalimbali nchini.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.