LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali ya Rais Samia yakabidhi nyumba 109 kwa wahanga wa tope Hanang Manyara

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kutekeleza azma ya kujali wananchi wake, Serikali makini ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeonyesha kujali na kuthamini maisha ya watanzania kwa kukabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko ya tope yaliyotokea Disemba 2023 kwa wakazi wa Kata za Katesh, Jorodom na Gendabi Hanang, mkoani Manyara.

Nyumba hizo za kisasa ilizojengwa katika eneo la Gidagamowd katika Kitongoji cha Waret, zimekebidhiwa kwa wananchi Disemba 20, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Majaliwa amesema mradi huo ni ushahidi wa dhamira ya Serikali kusaidia wananchi kurejea katika maisha yao ya kawaida baada ya kupoteza wapendwa wao, mali, na makazi yao ili waweze kuendelea na maisha yao kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya kupatwa na maafa hayo.

"Tunawapongeza wanufaika wote na tunatoa shukrani kwa wadau wote walioshirikiana kufanikisha mradi huu, Kwa pamoja tunaijenga Tanzania imara na yenye matumaini" amesema.
#KAZIINAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.