LIVE STREAM ADS

Header Ads

LVRLAC waibeba ajenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Watengenezaji wa majiko yanayotumia kuni mbadala wameombwa kuendelea kutoa elimu kwa watumuaji ili waweze kuona tofauti ya majiko hayo na majiko mengine ikiwemo gesi.

Ombi hilo limetolewa Alhamis Disemba 19, 2024 na Mratibu wa Jumuiya ya Mamlaka za Serikali za Mitaa Ukanda wa Ziwa Viktoria, Noela Levira wakati akizungumza kwenye kikao cha wanawake viongozi wa jumuiya hiyo na wauzaji wa majiko yanayotumia nishati mbadala.

"Watumuaji wakiwa na elimu ya kutosha juu ya matumuzi ya majiko hayo itasaidia jamii kuwa na mazingira rafiki na kupunguza uharibifu wa misitu katika nchi yetu" amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa LVRLAC, William Gumbo amesema wameanza kuchukuwa hatua za makusudi na watahakikisha wanahama kwenye mazowea na wanakwenda kwenye njia mbadala ya nishati safi .

"Tutaenda kuwa chachu kwenye halmashauri zetu kwa maana ya kutoa elimu na kuwa mbele kwa kuhakikisha kwamba tunakuwa chanzo cha mabadiliko kwa jamii yetu "amesema.

Kwa upande wake Katibu wa jumuiya hiyo, Billy Brown, amesema lengo la kukutana na wanawake viongozi Kanda ya Ziwa Victoria ni kujadili namna wanaweza kuwa na mikakati ya kufikia malengo ya taifa kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mmoja wa wauzaji wa majiko ya kuni mbadala ya ECOA, Bala Luhega amesema majiko hayo yanasaidia kupunguza uharibifu wa misitu pamoja na kulinda afya za za watumiaji kwani hayana moshi.
Mwenyekiti wa LVRLAC Kanda ya Tanzania, William Gumbo akizungumza kwenye kikao cha wanawake viongozi wa jmuiya hiyo.
Katibu Mkuu LVRLAC Kanda ya Tanzania, Billy Brown akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi Chabri Energy, Benard Makachia akizungumza kwenye kikao hicho.
Picha ya pamoja.
Washiriki wa kikao cha wanawake viongozi wa Jumuiya ya Mamlaka za Serikali za Mitaa LVRLAC Kanda ya Tanzania inayojumuisha Halmashauri zilizo mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria.
Majiko yanayotumia kuni mbadala.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.