Mradi wa Imarisha Wasichana waleta tija Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mradi wa Imarisha Wasichana unaotekelezwa na mashirika ya SAWAU na MIBOS kupitia ufadhili wa shirika la CRVPF kutoka Uganda, umetajwa kuwasaidia wasichana jijini Mwanza kujitambua, kuanzisha miradi ya kiuchumi na kuepusha matukio ya ukatili wa kijinsia.
Baadhi ya wasichana walionufaika na mradi huo kutoka mwaka 2019, wameeleza kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ushonaji nguo, mikoba na utengenezaji wa sabuni baada ya kujengewa uwezo na mashirika hayo ambapo hadi sasa zaidi ya wasichana 3,000 wamefikiwa na mradi huo.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: