LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la KIVULINI laendesha mdahalo wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI limeendesha mdahalo wa kuelimisha jamii kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia katika Wilaya ya Magu mkoani Mwanza huku msisitizo ukitolewa wanaume na wanawake kushirikiana katika mipango na maendeleo ya familia.

Mdahalo huo umefanyika Ijumaa Disemba 06, 2024 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani yanayofanyika kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 10, 2024 yakiwa na kaulimbiu isemayo, "kuelekea miaka 30 ya Beijing, chagua kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Katika mdahalo huo, baadhi ya wanawake walifichua kwamba siku hizi wengi hawatimizi wajibu wao wa kutunza familia na badala yake wamekuwa wakiwaambia wajiongeze ili familia ipate mlo.

Ilibainishwa kuwa baadhi ya wanawake wilayani Magu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto cha ukatili ikiwemo wa kiuchumi hasa wakati wa mavuno kutokana na wenza wao kutokomea na fedha wanapouza mazao na wanapohiji ndipo huambiwa wajiongeze.

Hata hivyo jitihada za kuelimisha jamii ambazo zimekuwa zikifanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo shirika la KIVULINI zimeanza kuzaa matunda.

Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mwaka huu yanaambatana na kaulimbiu isemayo, ‘kuelekea miaka 30 ya Beijing, chagua kutokomeza ukatili wa kijinsia”.

Katika kufanikisha hilo, Halmashauri ya Wilaya ya Magu ilizindua rasmi zoezi la kukabidhi vitambulisho vya wajasiriamali vilivyoboreshwa pamoja na utoaji mikopo ya asilimia 10 kwa vijana, wanawake na walemavu ili kuwasaidia kujikwamua na ukatili wa kiuchumi.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kushoto) akiwa na Afisa Mwandamizi wa shirika hilo, Grace Mussa (kulia) kwenye mdahalo wa kupinga ukatili uliofanyika Kaa ya Ng'haya wilayani Magu.
Katibu Tawala Wilaya ya Magu, Jubilate Lauwo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mau, Joshua Nasary (hayuko pichani).
Washiriki wa mdahalo huo wakimsikiliza Katibu Tawala Wilaya ya Magu, Jubilate Lauwo.
Wakazi wa Kata ya Ng'haya wakifuatilia mdahalo huo.
Katibu Tawala Wilaya ya Magu, Jubilate Lauwo akikabidhi vitambulisho vya wajasiriamali wadogo vilivyoboreshwa.
Katibu Tawala Wilaya ya Magu, Jubilate Lauwo akikabidhi vitambulisho vya wajasiriamali wadogo vilivyoboreshwa.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.