LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali ya Rais Samia kutatua changamoto ya maji Njombe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inakwenda kumaliza adha ya maji mkoani Njombe kupitia mradi wa miji 28.

Kiasi cha dola milioni 15 (sawa na shilingi Bilioni 40 za Kitanzania) zimetengwa kutumika kumaliza tatizo la upungufu wa maji katika kata tatu za Njombe, ambazo ni Ramadhani, Njombe Mjini, na Mjimwema.

Hadi ifikapo mwaka 2026 kuna uwezekano wa mradi huo wa maji kuwa umekamilika na unatekelezwa chini ya mpango wa serikali wa mradi wa maji wa miji 28, ambapo Njombe ni miongoni mwa miji inayonufaika.

Mradi huu utasaidia kuongeza upatikanaji wa maji kutoka lita milioni 5 kwa siku zilizopo sasa hadi lita milioni 17 kwa siku.

Katika ziara aliyoifanya Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Kisaa Kasongwa, Disemba 3, 2024, kwenye chanzo cha maji cha mto Hagafilo, ambacho kitazalisha maji kwa ajili ya mradi huu, amewahimiza watekelezaji wa mradi huo kutoa kipaumbele kwa wazawa wa Njombe katika nafasi za ajira na pia kununua vifaa vya kutekeleza mradi kutoka kwa wafanyabiashara wa ndani ya mkoa.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Njombe (NJUWASA), Mhandisi Robert Lupoja amesema kuwa mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo Aprili 2026.

Wananchi wa miji ya Njombe wanatarajia kupunguzwa kwa Ankara za maji mara mradi huo utakapo kamilika tofauti na wakati huu ambapo maji yanatolewa kwa mgao.
#KAZIINAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.