Serikali ya Rais Samia yagharamia Bilioni 1.4 kila mwezi Muhimbili
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwajali wananchi wake wasiokuwa na uwezo kifedha.
Hii ni kutokana na kugharamia matibabu ambapo Hospitali ya Taifa Muhimbili, hutoa msamaha wa gharama za matibabu za wagonjwa kati ya Shilingi Bilioni 1.2 hadi Bilioni 1.4 kila mwezi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof.
Mohamed Janabi amesema mbali na kiasi hicho kwa kila mwezi, kwa mwaka 2023 idadi ya wagonjwa wasiokuwa na uwezo iliongezeka ambapo ilifikia kugharamia Shilingi Bil.12 kila mwezi kwa wale wanaokidhi vigezo.
“Hizi fedha za hawa wanaolipa fedha taslimu ndo zinatusaidia kufidia kwa hawa wasiokuwa na uwezo kabisa, na katika malipo kuna aina nne za malipo, kwa fedha taslimu, kuna wanaolipa fedha taslimu ambao asilimia kubwa ni wa Bima hasa NHIF, wale wanaolipa nusu na nusu inalipwa na Muhimbili au Serikali” amesema Prof. Janabi.
Amesema kulipa gharama kwa wasiokuwa na uwezo kifedha, kunatumia kiasi kikubwa cha fedha na kuna wagonjwa ambao hao hawajiwezi kabisa hivyo ni lazima kuwagharamia.
“Ebu jaribu tu kufikiria kama tuna wagonjwa 4,000 na wasilipe chochote, hii hospitali itaweza kudumu kwa muda gani, naomba tukumbushane, Muhimbili ni Hospitali ya daraja la nne hivyo ukisikia kuna mgonjwa wa malaria Muhimbili ni yule mwenye hali ngumu, utakuta mpaka figo zimefeli hivyo anahitajika (Dylisis) na gharama yake inakuja mpaka Milioni 25" amesema.
#KAZIINAONGEA
No comments: