Jamii yakumbushwa kutowatenga waraibu wa dawa za kulevya
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Naweza Tena, Esther Morris ametoa rai kwa jamii kuondoa mtazamo hasi kuhusu waraibu wa dawa za kulevya na badala yake kuwasaidia ili kuondokana na changamoto hivyo.
Morris ametoa rai hiyo wakati akikabidhi zawadi mbalimbali za sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kwa waraibu wa dawa za kulevya wanaopata tiba ya methadone pamoja na mabinti walioacha biashara haramu ya ngono.
Katika jitihada za kuwasaidia kiuchumi waraibu wa dawa za kulevya na mabinti walioacha biashara haramu ya ngono, shirika la Naweza Tena lililopo Mtaa wa Msumbiji Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, limeanzisha mradi wa kuosha magari uitwao Millagro Car Wash katika eneo la Mission jijini Mwanza na kuwapa fursa ya kufanya kazi na kujipatia kipato.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: