Shirika la Peace For Conservation lakipiga jeki kikundi cha utalii
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Peace For Conservation limetoa mafunzo ya fursa na utalii endelefu kwa kikundi cha utalii cha Mwabulugu kilichopo Lamadi mkoani Simiyu.
Pia shirika hilo limekabidhi na vifaa okozi (life jackets) ili kuwezesha kikundi hicho chenye wanachama zaidi ya 60 kufanya shughuli za utalii wa kiutamaduni kwa weledi katika Ziwa Victoria, eneo la mwalo wa Mwabulugu ulio jirani na pori la Kijereshi na hifadhi ya Serengeti.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: