LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yaendelea kukuza sekta ya viwanda

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kuinua Sekta ya Viwanda kwa kujenga viwanda na kutoa fursa za Uwekezaji nchini sambamba na ajira, mkakati ambao umeanza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Hilo limeridhishwa na kiwanda cha vioo cha KEDA kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, kutokana na shughuli za uzalishaji zinazofanywa na kiwanda hicho, ambacho kimetoa fursa za ajira 800 kwa sasa, na kina mategemeo ya kutoa fursa 3,000 hapo baadae.

Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Tony Wu amethibitisha hayo na kusema kuwa, malengo ya kiwanda hicho ni kuwa kiwanda ambacho kinazalisha kioo bora ambacho kitaweza kutumika ndani na nje ya nchi.

Aidha, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo ametembelea kiwanda hicho kilichopo Mkuranga Jijini Dar es Salaam, na kuridhishwa na uzalishaji wa vioo na utoaji ajira, na kusema kwamba, Wizara ipo katika kusaidia malengo ya Rais Dkt.Samia ya Uwekezaji wa Viwanda nchini yanatimia na ndio maana Wizara imekuja na mpango wa ujenzi wa viwanda wa miaka sita katika mikoa na wilaya zote nchini.

Waziri Dkt.Jafo ametoa rai kwa wawekezaji nchini kuongeza wigo wa uwekezaji ili kuendeleza uchumi wa viwanda ndani ya nchi, ambapo amesema wamiliki wa viwanda wana haja kubwa ya kuitana nchini pamoja na kuongeza wigo wa uwekezaji wa viwanda kwenye maeneo mbalimbali yaliyopo nchini.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga Omary Mwanga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amesema, Uwekezaji wa kiwanda hicho umekuwa msaada mkubwa kwenye ajira kwa vijana, mapato ya Serikali lakini pia kushirikiana kwenye mambo ya kijamii.
#KAZIINAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.