LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mitambo nane mradi wa JNHPP yakabidhiwa serikalini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mitambo nane katu ya tisa ya kuzalisha umeme katika mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) tayari imekabidhiwa kwa Serikali baada ya kuwashwa na hivyo imebakia mashine moja tu ambayo itakuwa tayari mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.

Aidha Dkt. Biteko ametaja ongezeko la wadau ambao wako tayari kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa umeme Afrika na kupelekea Benki ya Dunia kutoa ahadi ya dola za kimarekani bilioni 22, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) dola bilioni 18.2, Benki ya Maendeleo ya Kiislamu dola bilioni 2.7, Benki ya Maendeleo ya Asia dola bilioni 1.5, Benki ya Maendeleo ya Ufaransa dola bilioni 1 na wafadhili wengine lukuki.

Dkt. Biteko aliyasema hayo Januari 31, 2025 Bungeni jijini Dodoma. Kazi Inaendelea. 

No comments:

Powered by Blogger.