LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wafanyabishara watakiwa kujisajili kwenye mfumo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali kupitia Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko ya Kariakoo, Hawa Ghasia amesema kuwa kuanzia Januari 31, 2025, majina ya wafanyabiashara 1,520 waliokuwepo soko la Kariakoo kabla ya ajali ya moto ya Julai 10, 2021, yatatangazwa ili wajisajili katika mfumo wa kidigitali wa TAUSI.

Mwenyekiti Ghasia amesema taarifa rasmi itatolewa mara baada ya kukamilika kwa upangaji wa kundi la kwanza la waliokuwapo awali.

Aidha amebainisha kuwa hakuna mfanyabiashara atakayerudi sokoni kabla ya kulipa deni lake la awali kwa kuwa kuna wafanyabiashara 366 wanadaiwa zaidi ya sh. milioni 358 kabla ya ajali ya moto, hivyo wanapaswa kulipa madeni yao kabla ya kupatiwa funguo za kurejea sokoni.

Soko la Kariakoo lilisitisha shughuli zake mwaka 2021 baada ya kuungua moto na sasa serikali imekarabati na kujenga jengo jipya kwa gharama ya Sh.Bilioni 28.03 na biashara zitarejea rasmi Februari mwaka huu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametangaza kuwa kuanzia Februari 22, 2025, biashara katika soko hilo zitaendeshwa saa 24.
KAZI INAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.