Rais Samia azindua Sera ya Elimu
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convertion Center ambapo Tanzania imeandika historia, katika uzinduzi huo Rais Samia amesema kuwa uamuzi huu wa kihistoria wa kuboresha sera na muundo wa elimu ya Tanzania unakusudia kulipatia Taifa vijana wenye elimu bora zaidi, wanaojiamini zaidi, na wenye nyenzo stahiki kushindana kikanda na kimataifa.
Ameongeza kuwa kazi ya msingi ya ujenzi wa miundombinu inayobeba utekelezaji wa sera na mabadiliko haya inaendelea, ambapo katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024 zimejengwa shule mpya za msingi 1,649, shule mpya za sekondari 1,042, vyuo 64 vya ufundi stadi (VETA) katika wilaya 64 ambazo awali hazikuwepo.
Hata hivyo Rais Samia ameelekeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Fedha, Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Mipango na Uwekezaji kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mabadiliko haya ili yaweze kuleta manufaa tunayokusudia.
Amesema utekelezaji huo unapaswa kwenda sambamba na kupitia upya maslahi ya kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahili kama mama wa taaluma zote duniani.
KAZI INAONGEA
No comments: