Shirika la MSICHANA TAI laadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Msichana Tai limeungana na wananchi, viongozi na wadau mbalimbali wa Serikali na taasisi binafsi kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ngazi ya Mkoa wa Mwanza, Alhamisi Machi 06,2025 katika uwanja wa Nyamagana.
Mwaka huu maadhimisho hayo Yana kauli mbiu isemayo "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji" ikiwa na lengo la kuhamasisha jamii kukuza usawa wa kijinsia, haki na uwezeshaji wa wanawake na wasichana.
Kwa upande wa shirika la Msichana Tai limekuja na ujumbe wa “Msichana Tai tunaimarisha haki, usawa uwezeshaji kwa mstakabali bora wa wanawake na wasichana”. Kilele cha maadhimisho hayo ni Machi 08,2025 kitaifa yakifanyika mkoani Arusha.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: