Nyamagana waadhimisha Siku ya Wanawake, Makilagi akemea ukatili wa kijinsia
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi amewataka watu wanaojihusisha na vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kuachana na tabia hiyo kwani Taifa la Tanzania linaongoza kwa usawa wa kijinsia.
Hayo ameyabainisha Jumanne Machi 04,2025 katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ngazi ya Wilaya ya Nyamagana yaliyoadhimishwa katika uwanja vya Nyamagana kwa kufanya matembezi, mazoezi, uvutaji kamba na kucheza mpira wa miguu.
Makilagi ameeleza kuwa hayo yalianzishwa kama njia ya kutambua na kusherehekea mchango ya wanawake katika jamii, kupigania haki zao na kuhusisha harakati za wanawake, haki za kiraia, kijamii na kiuchumi ambazo zilianza kuwa na nguvu mwanzoni mwa karne ya 20.
"Kama kweli kama kuna unyanyasaji unaendeleaje kwa wanawake au wanaume, kwa kipindi hiki tunachoendelea na maadhimisho haya tunaomba wanaofanya hivyo waachane na vitendo hivyo" amesema Makilagi.
Aidha Makilagi ameeleza kuwa kumekuwa na mikakatika mbalimbali ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia pamoja na ukatili majumbani kwa kuunda kamati kuanzia ngazi ya Mtaa hadi Wilaya.
"Tuna taasisi mbalimbali zinazoshirikiana na sisi kuhakikisha tunazuia vitendo hivyo vya ukatili, kila taasisi za umma na binafsi kuna madawati ya jinsia kwa ajili ya kusaidia kutokomeza vitendo hivyo" ameeleza Makilagi.
Naye Afisa Maendeleo Halmashauri ya Jiji la Mwana, Zena Kapama ameeleza kuwa wanaadhimisha mwendelezo wa siku ya wanawake duniani kufuatia wanawake wa New York nchini Marekani waliofanya maandamano wakidai haki zao baada ya kupata ujira mdogo kazini, kupunguziwa saa za kazi na kuboresha masharti ya kazi.
Ikimbukwe kuwa ifikapo Machi 08 kila mwaka, mataifa mbalimbali duniani huadhimisha siku ya wanawake duniani, huku kitaifa mwaka huu yakitarajiwa kufanyika jijini Arusha. Kwa Mkoa Mwanza maadhimisho hayo yatafanyika Machi 06, 2025 katika uwanja wa Nyamagana.
Na Chausiku Said, Mwanza




Viongozi, wadau na wananchi wilayani Nyamagana wameungana pamoja kuadhimisha Siku ya Wanawake Machi 04, 2025 ambapo kilele ni Machi 08, 2025 kitaifa mkoani Arusha huku kauli mbiu ikiwa ni "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji" ikiwa na lengo la kuhamasisha jamii kukuza usawa wa kijinsia, haki na uwezeshaji wa wanawake na wasichana.
No comments: