MWANZA: Kampuni ya Kiboko yafunga mashine ya kisasa ya kukata mabati, kuweka mikunjo
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kampuni ya MMI Steel iliyo chini ya makampuni ya Motisun Group inayozalisha mabati ya Kiboko imekuja na suluhisho kwa wateja wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, baada ya kufunga mashine ya kisasa wa kukata mabati na kuweka mikunjo ya aina mbalimbali katika Jiji la Mwanza.
Akizungumza Jumamosi Juni 21, 2025 jijini Mwanza kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo mafundi mbalimbali wakiwemo wa rangi, bati, nondo na bomba, Mkuu wa Masoko wa makapuni ya Motisun Group, Erhard Mlyansi alisema hatua hiyo itasaidia wateja kupata huduma bora kwa gharama nafuu.
"Awali mteja alikuwa hawezi kupata mabati kwa vipimo anavyohitaji hapa Mwanza, ilimlazimu asubiri mzigo utoke Dar es salaam jambo ambalo liliongeza gharama za usafirishaji na na muda wa kusubiri hivyo tumesikia maombi ya wateja wetu na kuyafanyia kazi" alisema Mlyansi.
Mlyansi alibainisha kuwa pia Motisun Group kupitia makampuni yake imekuja na bidhaa mpya mbalimbali ikiwemo za rangi, banti na mabomba hivyo mafunzo hayo yalilenga kutoa uelewa kwa mafundi jijini Mwanza ili kuwasaidia kutoa huduma bora kwa wateja.
Pia Mlyansi alibainisha kuwa ili kuendelea kupunguza gharama za upatikanaji wa bidhaa kwa wateja, Motisun Group ina mpango wa kujenga kiwanda cha mabomba na matanki jijini Mwanza ili kuwapunguza gharama za usafirishaji kwa wateja wa Kanda ya Ziwa wanaotegemea bidhaa hizo kutoka Dar es salaam.
Baadhi ya mafundi waliohudhuria mafunzo hayo wakiwemo Emmanuel Kibalya, Peter Odila na Jackline Mwita walisema teknolojia inabadilika kila siku hivyo elimu waliyoipata itawasaidia kufanya kazi kwa weledi huku wakiwa mabalozi wazuri wa bidhaa za Motisun Group.
"Naishukuru kampuni ya Kiboko, wamefunga mashine nzuri ambayo itanirahisishia kupata mabati kwa kipimo ninachokita hapa hapa Mwanza" alisema Kibalya.
Naye Odila alisema "nimeanza upakaji rangi tangu mwaka 1989, mafunzo haya yanatuongezea ujuzi kwa sababu teknolojia ya ujenzi na upakaji rangi inabadilika kila siku. Changamoto tulizokuwa tunakutana nazo tunafurahi kwamba tutaenda kuzitatua".
Zaidi ya mafundi 200 walishiriki mafunzo hayo yaliyofanyika eneo la Nyakato Steel jijini Mwanza na kutunukiwa vyeti.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Masoko wa makapuni ya Motisun Group, Erhard Mlyansi akizungumza kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo mafundi jijini Mwanza.
Mafunzi mbalimbali jijini Mwanza wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa na Motisun Group.
Mafunzi mbalimbali jijini Mwanza wakifuatilia mafunzo.
Afisa Masoko kampuni ya Motisun Group, Ezekiel Sanga akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Mauzo kampuni ya Kiboko Plastics, Yassin Ausi akielezea ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo ikiwemo matenki na mabomba.
Afisa Mauzo Motisun Group, Frank Katumwa akizungumza wakati wa mafunzo hayo na kuwasihi mafunzi kuendelea kutumia bidhaa mbalimbali za chapa ya Kiboko ikiwemo rangi, nongo na mabati.
Mmoja wa mafunzi wakongwe jijini Mwanza walioshiriki mafunzo hayo, Peter Odila akitoa shukurani kwa Motisun Group kwa kuendelea kuwajengea uelewa ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia ya ujenzi.
Mshiriki wa mafunzo hayo Peter Odila akitoa shukurani kwa Motisun Group kwa kuendelea kuwajengea uelewa ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia ya ujenzi.
Mkuu wa Masoko wa makapuni ya Motisun Group, Erhard Mlyansi (kushoto) akimfafanulia jambo mmoja wa mafundi waliohudhuria mafunzo hayo, Peter Odila (kulia).
Mkuu wa Masoko wa makapuni ya Motisun Group, Erhard Mlyansi (kulia) akielekeza jambo wakati wa mafunzo kwa mafundi jijini Mwanza.
Kutoka kushoto ni Meneja kiwanda cha bidhaa za plastiki za Kiboko- Rajendra Baber, Meneja kiwanda cha mabati ya Kiboko- Partha Pattanayak- Afisa Masoko bidhaa za plastiki- Yassin Ausi, Meneja wa kiwanda cha rangi za Kiboko- Mohamed Zameer na Stock Meneja- Mansukh Dabasiya.
Meneja kiwanda cha bidhaa za plastiki za Kiboko- Rajendra Baber (kulia) akikabidhi vyeti kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Afisa Masoko bidhaa za plastiki- Yassin Ausi (kulia) akikabidhi vyeti kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Mwonekano wa bidhaa mbalimbali ikiwemo mabati zinazozalishwa na makampuni ya Motisun Group.
Mwonekano wa bidhaa mbalimbali ikiwemo rangi zinazozalishwa na makampuni ya Motisun Group.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: