LIVE STREAM ADS

Header Ads

WASHINDI KAMPENI YA "ORYX GESI YENTE" WAKABIDHIWA ZAWADI JIJINI MWANZA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Washindi wa kampeni ya Gesi Yente inayoendeshwa na kampuni ya Oryx Enegies kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia wamekabidhiwa zawadi zao jijini Mwanza.

Hafla ya kukabidhi zawadi hizo imefanyika Jumanne Septemba 02, 2025 katika ofisi za Wakala wa Oryx Buhongwa na kuongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala aliyemwakilisha Mkuu wa Wikaya hiyo, Amina Makilagi.

Katika salamu zake, Salala amepongeza kampuni ya Oryx kuja na kampeni hiyo inayounga mkono jitihada za Serikali kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi na kuachana na matumizi ya nishati chafu ikiwemo kuni na mkaa kutokana na madhara yake.

Salala amesema elimu unayoendelea kutolewa na Serikali kwa kushirikiana na wadau imeanza kusaidia wananchi kutumia nishati safi ambayo ni rafiki kwa mazingira na kiafya kwa watumiaji.

 Naye Meneja Mkuu wa Mauzo na Masoko ORYX Tanzania, Shaban Fundi amesema kupitia kampeni hiyo, mteja akinunua gesi ya Oryx anapata kuponi ambayo ndani yake kuna zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki, baiskeli, majiko, sufuria, mabegi na chupa za maji.

Fundi amesema kampeni hiyo inalenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuokoa Taifa kuwa jangwa kutokana na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa, ambayo ni nishati chafu yenye madhara ya kiafya kwa watumiaji.

Akizungumza baada ya kupokea zawadi ya pikipiki, Maximilian Nyamoge amesema alihamasika kutumia nishati ya gesi kwa sababu haina usumbufu wakati wa kuwasha kama kuni na mkaa na kwamba inawahisha mapishi.

Jumla ya washindi watatu wamekabidhiwa zawadi kupitia kampeni hiyo ya Gesi Yente iliyoanza Agosti  13, 2025 ambapo mmoja amepata pikipiki na wawili baiskeli.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala akizungumza kwenye hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa kampeni ya Oryx, Gesi Yente kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi (hayuko pichani).
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala akizungumza kwenye hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa kampeni ya Oryx, Gesi Yente
Meneja Mkuu wa Mauzo na Masoko Oryx Tanzania, Shaban Fundi akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika Buhongwa jijini Mwanza.
Mfanyakazi wa Oryx akitoa elimu ya usalama wa gesi wakati wa hafla hiyo.
Elimu kuhusu matumizi sahihi ya gesi ikitolewa kwenye hafla hio.
Hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa kampeni ya Oryx Gesi Yente imefanyika Buhongwa jijini Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala akikabidhi baiskeli kwa mshindi.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala akikabidhi baiskeli kwa mshindi.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala akikabidhi pikipiki kwa mshindi.
Mshindi akionyesha kadi ya pikipiki.
Kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupitikia kupitia gesi ya Oryx iitwayo Gesi Yente ilianza Agosti 13, 2025 na zawadi mbalimbali zinatolewa kwa wateja.

No comments:

Powered by Blogger.