TASAF WATAKIWA KUFANYA TATHMINI KAYA MASKINI TANZANIA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa ameuagiza Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini kuhakikisha wanafanya tathimini na kuja na mapendekezo kwa Serikali juu ya upungufu wa kaya maskini nchini.
Majaliwa alibainisha hayo Septemba 11, 2025 jijini Mwanza wakati akikagua maendeleo ya taasisi mbalimbali nchini katika kongamano la nne la ufuatiliaji, tathimini na ujifunzaji.
Alisema takwimu zinaonesha kuwa idadi kubwa ya kaya zinaoneka kuondokana na umaskini kila kukicha hivyo ipo haja ya mfuko huo kuja na ushauri juu ya kipi serikali hususani pale kaya masikini zinapoonekana kupungua nchini.
“Takwimu zinaonesha wengi wame ‘graduate’ hivyo hali ya umaskini imeshuka, nini tathimini yenu pengine umaskini unaisha au la” alisema Majaliwa.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema Rais Samia Suluhu Hassan anaamini katika tathimini na kuwa ni maelekezo yake zifanyike kwa ukamilifu na kila taasisi ya umma ili kuhakikisha Dira ya Taifa ya Maendelo ya mwaka 2025/50 inatekelezwa ipasavyo.
Alisema hatua hiyo itasaidia matokeo ya utekelezaji wa dira hiyo yanaweza kupimika mbele ya umma wa watanzania kupitia tathimini na uratibu na kuhakikisha yanaleta manufaa kwa watanzania wote.
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji, Tathmini, Mifumo na Mawasiliano kutoka TASAF, Japhet Boaz alisema tathimini inasaidia kuona hali ya umasikini ilivyo nchini na kubaini kuwa juhudi za kuondoka hali hiyo na siyo za kufanya na kuacha.
Alisema licha ya umaskini kuendelea kupunguzwa aushi, hivyo ni juhudi endelevu hasa katika kukabiliana na changamoto kubwa zinazowakabili Wananchi.
Alisema mpaka sasa wamefika asilimia nane pekee kati ya kumi za maskini wanaotajwa kuwepo nchini kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 hivyo juhudi za kuhakikisha maskini wanainuliwa zinaendelea.
“Hatuwezi kusema sasa umaskini umeisha hivyo mpango usitishwe bali lazima uwepo kwani kuna wakati yanatokea majanga na kuipua maskini wapya ambao wanahitaji msaada wa serikali” alisema Boaz.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi alisema Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za elimu imefanikiwa kuratibu mafunzo maalum kuhusu Ufuatiliaji na Tathimini kwa maofisa wakuu wa vitengo 781 kutoka Ofisi mbalimbali nchini.
Alisema hatua hiyo ni mkakati mkubwa unaolenga kujenga uwezo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathimini ambao serikali inautambua na kuuthamini.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: