LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAJALIWA AFUNGUA KONGAMANO LA UFUATILIAJI, TATHMINI NA KUJIFUNZA 2025

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majiliwa amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan katika kongamano la nne la ufuatiliaji, tathimini na ujifunzaji lililofanyika mkoani Mwanza.

Akizungumza katika kongamano hilo Mhe. Kassim Majaliwa amesema Mhe.Rais anaamini kuwa kongamano hilo litakuwa chachu na kuleta hamasa na kuhakikisha kuwa Dira ya Taifa ya Maendelo yam waka 2025/50 itatekelezwa na matokeo yake yanaweza kupimika mbele ya umma wa watanzania kupitia tathimini na uratibu na kuhakikisha yanaleta manufaa kwa watanzania.

Aidha ameleza kufurahishwa na kauli mbiu ya mwaka huu isemayo kuimarisha uwezo wa ufuatiliaji na tathimini kwa jamii ili kuimarisha utendaji kazi kwa maendeleo endelevu.

Amesema endapo wadau wote pamoja na jamii wakiwa na uelewa kuhusu shughuli za ufatiliaji na tathimini, Taifa litakuwa na matokeo makubwa na ya haraka.

“Kwa msingi huo ipo haja ya kuweka mikakati mahususi ya kuhakikisha kuwa jamii na watendaji wanajengewa uwezo kuhusua ufatiliaji na tathimini ili kuwezesha kila sekta kufanya tathimini ya kina” amesema.

Aidha ameeleza kufarijika na sehemu kubwa ya maelekezo aliyoyatoa katika makongamano matatu yaliyopita kuwa yametekelezwa kwa kiasi kikubwa hivyo kuwapongeza Waziri, Katibu Mkuu na wadau wengine waliowezesha utekelezaji huo.

Mhe. Majaliwa amesema serikali imeendelea kufanya jitihada katika kuhakikisha inaimarisha mifumo ya ufuatiliaji na tathimini ili kufikia malengo mbalimbali Taifa liliyojipangia.

Aidha amesema serikali imeongeza uwajibika wa mtu mmoja mmoja mahali pa kazi, uwazi na kasi katika kutenda, kasi katika utoaji huduma na ustawi wa wananchi.

Aidha amezielekeza idara zote zenye dhamana kuhakikisha zinakamilisha maandalizi ya sera ya serikali na tathimini ili iweze kutungwa sheria itakayoongoza ufuatiliaji na tathimini.

Kadhalika ameitaka ufuatilia wa mfumo wa kielectroniki utakaokuwa mfumo mkuu wa mifumo yote ya ufuatiliaji na tathimini ya uendeleaji ndani ya serikali ili kuzifuatilia vizuri idara za serikali.

781 Wapata Mafunzo Maalum ya Ufuatiliaji na Tathimini Nchini
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi amesema Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za elimu imefanikiwa kuratibu mafunzo maalum kuhusu Ufuatiliaji na Tathimini kwa maofisa wakuu wa vitengo 781 kutoka Ofisi mbalimbali.

Mhe.Lukuvi amebainisha hayo leo Septemba 11, 2025 mkoani Mwanza katika Tamasha la nne la Ufuatiliaji, Tathimini na Ujifunzaji lililofunguliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Aidha amesema Wakuu hao wanatoka Wizara mbalimbali, Taasisi, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri pamoja na Wadau kutoka nje ya nchi.

Amesema hatua hii ni mkakati mkubwa unaolenga kujenga uwezo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathimini ambao serikali inautambua na kuuthamini.

Pamoja na hayo, Mhe. Lukuvi amesema Serikali imefanikiwa kuanza ujenzi wa mfumo wa Kitaifa wa Kieletroniki wa Ufuatiliaji na Tathimini ambao utapokea taarifa kutoka mifumo miningine na kuzichakata na kuwezesha maandalizi ya taarifa ya utekelezaji wa serikali.

“Uwepo wa mfumo huo utawezesha kupokea data, kuzichakata, kuzitafsiri kwa wakati na kuiwezesha Serikali katika ngazi zote kutumia takwimu sahihi katika kupanga kuboresha afua zinazotekelezwa na kuamua kwa usahihi” amesema Mhe.Lukuvi.


Serikali, Taasisi za elimu zashirikiana kuimarisha wataalamu wa tathimini na ufuatiliaji
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri (Sera Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi, amesema Serikali imeendelea kushilikiana na Taasisi mbalimbali za elimu nchini katika kuhakikisha inaimarisha wataalam wa Tathimini na Ufuatiliaji Nchini.

Dkt. Yonazi amebainisha hayo Septemba 11, 2025 katika Kongamano la 4 la Ufuatiliaji, Tathimini na Ujifunzaji lililoongozwa na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa.

Akieleza jukumu la Ufuatiliaji na Tathimini katika utendaji kazi wa Serikali, Mhe.Yonazi amesema jukumu kubwa la kufanya Ufuatiliaji na Tathmini ni kukuza uelewa na kuimarisha utaalam katika kipindi ambacho ulimwengu na taaluma zote zimejikita katika matumizi ya akili unde ‘Artificial Interagency’.

"Hii ni fursa pekee ambayo inatukutanisha na Mataifa mbalimbali na kukuza utaalam, kadhalika inasaidia kuutangaza Utalii hasa kwa wageni kutoka nchi za nje" amesema Dkt. Yonazi.

Aidha amesema mada zinazoendelea kujadiliwa katika Kongamano hilo zitaibua mbinu na mijadala juu ya dhama na kuendelea kukuza Utendaji wa Serikali na kusaidia Sekta Binafsi kujifunza kupitia kupitia Idara na vitengo vya Serikali vinavyoshughulikia masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini.

Ameendelea kusema, Serikali imeendelea kukuza juhudi za kuongeza Wataalam katika kukuza Idara ya Ufuatiliaji ndani na nje ya nchi ili kuifanya nchi kuwa kuwa kituo cha kujifunza na kufundishia.

Aidha amesema Serikali kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za Elimu imeendela kutoa mafunzo kwa wataalam mbalimbali ili kuhakikisha nchi inakuwa na wataalam bora katika suala la Ufuatiliaji na Tathmini.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.