LIVE STREAM ADS

Header Ads

DKT. KIKWETE ASHIRIKI MKUTANO WA AUDA-NEPAD NCHINI ETHIOPIA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mheshimiwa Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu Duniani (Global Partnership for Education - GPE), ameshiriki katika Mkutano wa Ngazi ya Juu ulioandaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Umoja wa Afrika (AUDA-NEPAD), Addis Ababa, Ethiopia.

Mkutano huu uliohusu Mpango wa Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi barani Afrika (STISA 2034), ulikutanisha wadau mbalimbali barani Afrika na zaidi, kujadili mchango wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi katika maendeleo barani Afrika.

Rais Mstaafu Kikwete alisisitiza katika hotuba yake kuwa elimu ni msingi wa maendeleo na kuwa ni muhimu nchi wanachama wa Umoja wa Afrika waweke kipaumbele katika kutenga rasilimali za kutosha katika sekta ya elimu kwani kufanya hivyo kutawezesha matumizi ya kisasa ya Sayansi na Teknolojia na hatimaye kupelekea uvumbuzi kwa maendeleo ya nchi moja moja na bara la Afrika kwa ujumla.

“Elimu huwapa watu maarifa na ujuzi wa kushughulikia mahitaji na changamoto za kimaendeleo za Taifa na jamii kwa ujumla…na kwamba nchi zilizoendelea zaidi, zimewekeza sana katika elimu, sayansi na teknolojia” alisema Rais Mstaafu.
Rais Mstaafu wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

No comments:

Powered by Blogger.