Director Tyson wa Bongo Movie Afariki dunia......Aacha mwendelezo wa Simanzi kwa Wapenzi wa Bongo Movie hapa nchini.
![]() |
Gari alilopatanalo ajali Director Tyson |
"Baada
ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show
mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni ikiwa ni saa 4 tu toka tuanze
safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia
GAIRO mjini" Ilieleza taarifa ya Dj Choka na kuongeza...
"Kwenye
gari walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha ila wengine
wamepata majeraha mwilini akiwemo dereva wa gari hilo ambapo kwa sasa
mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa
Morogoro baadae asubuhi safari ya kurudi Dar es Salaam itaanza".
Ajali hiyo inaelezwa kuwa ajali mbali ambapo baadhi ya majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matibabu.
![]() |
Gari alilopatanalo ajali Director Tyson |
MTANZANIA MEDIA TUNATOA POLE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WALIOGUSWA NA MSIBA HUU. R.I.P TYSON ......Info. Kwa ushirikiano na Dj Choka.
No comments: