LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWONGOZAJI NA MWIGIZAJI MAHIRI BONGO MOVIE ADAM KUAMBIANA AFARIKI DUNIA.

Kuambiana enzi za Uhai wake
Ni vigumu kuamini kutoa taarifa kuwa yule muongozaji filamu maarufu ambaye vilevile ni mwigizaji wa filamu katika soko la Bongo Movie, Adam Kuambiana kuwa amefariki dunia.

Adam Kuambiana amefariki dunia jana wakati akipelekwa katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa matibabu alfajiri ya kuamkia hiyo jana.

Inatajwa kuwa kabla ya kuzidiwa marehemu alianguka chooni akiwa location katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remy jijini humo ambapo kabla ya mauti kumfika, Adam alikuwa akilalamika kuwa anasumbuliwa na tumbo.

Kwa hivi sasa mwili wa marehemu uko katika mochwari za hospitali hiyo, ukisubiri taratibu nyingine za mipango ya kifamilia hatimaye kupumzishwa katika nyumba yake ya milele.
 
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

No comments:

Powered by Blogger.