MAHUSIANO: NI KUBAYA...MKE WA TYSON ATAKA MALI ZAKE.
Wakati hata siku arobaini hazijatimia, mke wa marehemu George Otieno ‘Tyson’, Beatrice Shayo juzi alicharukia mali zake baada ya kuamua kutinga nyumbani kwa marehemu, Mbezi Makonde jijini Dar kwa lengo la kuchukua kila kinachomhusu.
Mdada huyo aliyefunga ndoa na Tyson Agosti
9, 2012 nchini Kenya na kujaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye
Eugene, alishuhudiwa na gazeti hili Juni 24, mwaka huu saa sita usiku
akiwa na ndugu zake na kuanza kugonga geti la nyumba hiyo.
Katika kujua kilichokuwa kikiendelea, mmoja
wa mapaparazi wetu aliwasogelea na kuzungumza na Beatrice ambaye
alieleza kuwa, lengo lake lilikuwa ni kuchukua mali zake zilizomo mle
ndani.
“Ulidhani mimi nataka kuingia kwenye nyumba
hii nikae, la hasha! Nimefuata mali zangu tu basi,” alisema Beatrice
huku akiendelea kugonga geti hilo.
Wakati Beatrice na nduguze wakionekana
kukata tamaa ya kufunguliwa, mara alitokea mwanamke anayedaiwa alikuwa
akiishi na marehemu mpaka kifo kilipomkuta na kuuliza aliyegonga geti ni
nani, alipotajiwa jina la Beatrice alisema: “Eee, Beatrice, usiku huu
umekuja kutafuta nini?”
Beatrice: Nina shida, naomba ufungue tuongee.
Mwanamke: Hatuwezi kuongea usiku huu, uje kesho asubuhi.
Beatrice: Nakuomba ufungue tu, nimekuja kuchukua mali zangu nilizoacha humo ndani na nimekuja na gari kabisa la kubebea.
Mwanamke: Mali gani, humu hamna chako na kama una kitu chako humu, fuata taratibu.
Beatrice: Nimefuata taratibu, nipo na mjumbe hapa.
Mwanamke: Ndiyo nasema mje kesho asubuhi na mapema mtanikuta.
Baada ya mwanamke huyo kugoma kufungua,
mjumbe wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la Sabina Mawanda aliwashauri
waondoke na kurudi tena asubuhi lakini inadaiwa walipofanya hivyo
walikuta nyumba imefungwa na hakukuwa na mtu.
Na:Global Publishers.
No comments: