MICHEZO: GHANA NA URENO WAYAAGA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA.
Ronaldo alifunga bao la ushindi dhidi ya Ghana
Cristiano Ronaldo aliifungia
ureno bao la ushindi timu yake ilipoilaza Black Stars ya Ghana 2-1
katika mechi ya mwisho ya makundi. Tatizo ni kwamba Ureno ilikuwa imeishabanduliwa nje ya kipute hicho baada ya kushindwa mechi zao za kwanza.
Ronaldo hata hivyo atamshukuru kipa wa Ghana Fatawu Dauda kwa sifa alizopata baada ya kufunga bao la ushindi kufuatia kipa huyo kumzawadia mpira katika eneo la lango naye akaifuma kimiani.
Ghana ilikuwa bila Muntari na Boateng ilipochuana na Ureno
Ghana hata hivyo ilikuwa tayari inakumbwa na kashfa ambayo wachezaji wake wa kutegemewa Kevin Prince Boateng na Sulle Muntari walitimuliwa kambini huku wale waliosalia wakitishia kususia mechi hiyo ya Ureno kufuatia ubishi kuhusiana na malimbikizi ya marupurupu yao.
Na: bbcswahili.
No comments: