WAFARIKI KWA KUFUKIWA NA MAWE WAKITAFUTA RUPIA ZILIZOACHWA NA WAKOLONI MKOANI MWANZA.
![]() |
Shimo ndilo hili |
Tukio hilo lilitokea Jaza asubuhi
(Jumatano) ambapo hadi kufikia jana Mwili wa Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Zubery
Kaima (45) ulishindwa kupatikana mara baada ya juhudi za wananchi na Serikali
ya Wilaya ya Ilemela kushindikana kutokana na Kukwamishwa na Miamba
iliyozunguka katika eneo hilo la tukio.
Akizungumzia Tukio hilo, Bi.Zuwena
Khamis ambae mme wake alipoteza maisha katika tukio hilo ameeleza kuwa alipokea
taarifa za watu kufukiwa na miamba katika eneo hilo la Kangae B na alipofika
katika eneo hilo alikuta tayari mmewe Sufian Khamis amekwisha poteza
maisha.(Mwili wa Sufiani ulifanikiwa kufukuliwa siku ya jana).
Wakizungumzia Tukio hilo baadhi ya
wananchi wa Mtaa huo wa Kangaye B wamesema Kuwa chanzo cha Tukio hilo ni Imani
Potofu ambapo walidai kuwa mmoja wa hao waliopeza maisha alidai Kuoteshwa na
Mungu kuwa eneo hilo lina mali ambazo ziliachwa na Wakoloni wa Kijerumani.
![]() |
Wananchi wakiwa katika eneo la Tukio. |
Kwa Upande wake Sultan Said ambae
ni Mmoja wa Watu waliongia katika Mashimo ya Miamba hiyo kwa ajili ya Kujaribu
kuutafuta mwili wa Sufian Khamis ambae juhudi za kuutafuta mwili wake
zilishindikana, alisema kuwa walishindwa kuupata mwili huo kutokana na kuwa
katika Miamba Miamba ya Mawe yenye Upenyo mdogo usioweza kuruhusu binadamu
kuingia huku akiongeza kuwa pamoja na jitihada kubwa walizotumia wakiwa na
Tochi kuutafuta mwili huo lakini bado hawakuuona mwili huo.
Akizungumzia Tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya
Ilemela Amina Masenza aliwataka Wakazi na wananchi wa eneo hilo kuacha kuamini
mambo ya kufikirika na yasiyo ya kweli ambayo yanaweza kuleta hatari katika
maisha ya binadamu na hivyo kuwasihi kuwa ni vyema wawe wepesi wa kutoa taarifa
katika mamlaka husika pale wanapoona vitendo visivyo vya kawaida katika jamii.
Tukio hilo la Kusikitisha
lilitokea Juzi asubuhi mara baada ya Watu hao kuingia katika Shimo hilo lenye Miamba katika eneo la Kangaye B Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa lengo la
Kufuatilia MALI ambazo zimeelezwa kuwa Ziliachwa na Wakoloni wa Kijerumani
katika Mashimo yaliyo katika eneo hilo.
NA: HALITH JAHA ALLY.
No comments: