LIVE STREAM ADS

Header Ads

HABARI KAMILI KUHUSIANA NA KIVUKO CHA AJABU KILICHOZINDULIWA JIJINI MWANZA NA DK.MAGUFULI.

Waziri wa Ujenzi Mh.Dk.John Pombe John Magufuli.
Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli leo amezindua Kivuko Kipya Jijini Mwanza, ambacho kitakuwa Kikifanya Safari zake katika Mwambao wa Ziwa Victoria kwa lengo la Kupunguza adha ya Usafiri kwa wananchi kutokana na Msongamano wa Magari katikati ya Jiji.

Kivuko hicho ambacho kimepewa jina la MV.TEMESA kimegharimu fedha za Kitanzania zaidi ya Shilingi Milioni 640 kitakuwa Kikifanya Safari zake Kuanzia Eneo la Sweya kupitia Butimba TCC, Mkuyuni, Igogo hadi Kirumba huku Matarajio ya baadae yakiwa ni kuongeza safari za kivuko hicho Igombe na Kayenze.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo.
Akizungumza katika Uzinduzi huo, Dk.Magufuli alisema kuwa Kivuko hicho kitakuwa Mkombozi wa kweli kwa Wananchi wa Jiji la Mwanza, kwa kuwa kitawawezesha kuepukana na Msongamano wa Magari barabarani ambao hujitokeza katikati ya Jiji la Mwanza hususani nyakati za asubuhi na jioni.
                                  Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza (CCM) Stanslauns Mabula. 
Akitoa taarifa kuhusiana na Kivuko hicho, Celina Magesa ambae ni Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA, alisema kuwa kivuko hicho kimekarabatiwa kulingana na Viwango vinavyokubalika Kimataifa sanjari na kufanyiwa Ukaguzi na Mamlaka husika na hivyo kuthibitishwa kuwa kina Uwezo wa Kubeba abiria 80 na magari madogo matano ikiwa ni sawa na Tani 65.
Awali akimkaribisha Dk.Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo ameiomba TEMESA kuweka wazi ratiba za usafiri za Kivuko hicho sanjari na kuiomba Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuyabainisha maeneo ambayo kivuko kicho kitakuwa kikipita ili TEMESA iweze kukamilisha Ujenzi wake mapema huku akimuomba Waziri Magufuli kuongeza Kivuko kingine ili kiwe kinapishana na kivuko hicho kwa wakati mmoja.

Aidha amemuomba Waziri Magufuli kujenga daraja la watembea kwa Miguu katika eneo la Furahisha ili kuondoa kero ya Msongamano wa magari unaotarajiwa kuongezeka katika eneo hilo, hasa mara baada ya ujenzi wa jengo la Kimataifa la biashara la Mwanza Compelex kukamilika mwaka huu.
Baada ya Ombi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa juu ya Ujenzi wa Daraja la watembea kwa Miguu kama lililojengwa eneo la Mabatini kujengwa katika eneo la Furahisha Mkoani Mwanza, Ikamlazimu waziri Magufuli kutoa majibu yake ambapo alisema kuwa;
"Ndugu zangu wanamwanza kuna maombi yametolewa hapa, Diwani ametoa maombi, Mkuu wa Mkoa ametoa maombi, katibu wa CCM ametoa maombi, mwenyekiti wa CCM ametoa maombi, Mbunge wenu hajatoa maombi...kwa hiyo hao ndio wanaomsemea. Sasa mimi nataka niwaeleze kwamba maombi yenu nimeyapokea na nataka nikuahidi Mh.Meya na Mh. Mkuu wa Mkoa na wanamwanza wote kwamba daraja hilo tutalijenga ili hata wale wanaopenda kuandamana wawe wanaandamania katika madaraja hayo...".

Mv.Temesa Ambacho ni Kivuko kilichozinduliwa na Dk.Magufuli. Kivuko hiki kinaelezwa Kuwa Kivuko cha Kwanza Nchini Tanzania Kuwa na mwendo kasi zaidi kuliko Vivuko vyote hapa nchini na hivyo kufanya Kivuko hiki kuwa Kivuko cha AJABU NA CHA PEKEE kulivyo Vivuko vyote hapa nchini Huku huku jambo la Kujivunia likiwa ni kwamba Kimejengwa na Mkandarasi Mzalendo kutoka Mkoani Mwanza anaefahamika kama MS-Songoro Marin Transport ambayo ni Kampuni ya Kizalendo kabisa. Kivuko hiki kiko chini ya Usimamizi wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA.
Umati wa Watu ulijitokeza kwa wingi ili kuonja utamu wa kivuko hiki kwa mara ya kwanza baada ya kuzinduliwa, hapa wakishuka baada ya safari fupi ya Ziwani.
Sweya kwa mbaaaali.Hapa ndipo kivuko kitakuwa kikianzia safari zake kwenda maeneo ya town.
"Huu ndio Usafiri tuliokuwa tukiutegemea hapo awali, lakini sasa ni Mwendo wa Kivuko na Hii Mitumbwi itabaki kwa ajili ya Shughuli za Kiuvuvi".
Wanakwaya waliokuwa wakitoa burudani katika uzinduzi huo.

No comments:

Powered by Blogger.