LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA, LAKINI HIKI NDICHO KILICHOJILI KATIKA MKUTANO WA VIJANA MKOANI MWANZA.




Washiriki wa Mkutano wa Vijana Mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya Kuadhimisha siku ya dadi ya Watu Duniani inayotarajiwa Kuadhimishwa Kesho July 11. Mkutano huu umefanyika kwa Ushirikiano Mkubwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) na Wadau wengine kama Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini ( RITA) chini ya Uratibu wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango.

Imeelezwa kuwa ili kupata Mafanikio yanayotokana na Uwekezaji kwa Vijana, ni mhimu kuwa na Mpango Mkakati unaolenga Kuwekeza kwa Vijana katika Maeneo yenye Umuhimu kwa Vijana.

Hayo yameelezwa hii leo Mkoani Mwanza na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Marcella Mayala kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, wakati akifungua Mkutano wa Vijana ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Duniani ambayo inatarajiwa kuadhimishwa Kesho Mkoani Mwanza.



Mayala aliyabainisha Maeneo ambayo yanapaswa kupewa umhimu kwa vijana kuwa ni pamoja na eneo la Elimu, Utawala bora, Afya ya Uzazi pamoja na Uzazi wa Mpango.

Alisema kuwa Serikali inatilia Mkazo mkubwa katika kuwekeza kwa vijana wa kike na wa kiume ili kuwawezesha kushiriki na kuchangia katika shughuli za kujiendeleza kielimu na kiuzalishaji mali ili kuchangia katika pato la Taifa na ngazi ya familia kwa ujumla.


Katika Mkutano huo vijana kutoka Shule na Vyuo mbalimbali Mkoani Mwanza walikutana na kujadili kwa kina Fursa na Changamoto zilizopo kwa vijana, kwa lengo la kupata mapendekezo yatakayosaidia kuboresha Sera, Mikakati na Mipango ya nchi katika kupanga na kuelekeza matumizi ya rasilimali za nchi katika kuwekeza kwa vijana.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Idadi duniani mwaka huu Inasema “Wekeza kwa Vijana” ambapo inalenga katika kutambua umuhimu wa kuwekeza kwa vijana ili waweze kutoa mchango wao kwa maendeleo stahiki ya Taifa.


                       Julius Kiveli ambae ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam.


Akitoa Mada katika Mkutano huo, Dr.Julius Kiveli ambae ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam alibainisha kuwa katika Kuadhimisha Siku ya Idadi ya Watu duniani, haitoshi tu kuangalia idadi ya watu kwa wingi wao, pasipo kuhusisha idadi ya watu wenye elimu, afya bora na wenye uwezo wa uzalishaji katika jamii kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Victoria Mushi kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini ( RITA).

Marcella Mayala, Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana. "Napenda kuchukua fursa hii kutoa Mwito kwa Vijana wote wa kike na wa kiume kujituma katika shughuli zote wanazohusika nazo ikiwa ni pamoja na kupanua fursa kwa nchi yetu imejaliwa kuwa na fursa nyingi katika sekta mbalimbali za uchumi. Maendeleo ya nchi huanza na mtu mmoja mmoja, hivyo ni mhimu kwa kila kijana kujituma bila kusukumwa katika kuboresha maisha yake ya sasa na ya baadae" Alisema Mayala.

Pia masuala ya mbalimbali yamejadiliwa katika Mkutano huo ikiwa ni pamoja na Changamoto za Idadi ya Watu na Maendeleo, Fursa na changamoto zilizopo katika kuwawezesha vijana na Sanjari na Ndoa za Utotoni na masuala mengine mbalimbali yanayowahusu vijana.






Edwin Ninde ambae ni Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

Washiriki wa Mkutao huo kutoka Shule za Sekondari na Vyuo mbalimbali Mkoani Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.