LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU MKUU OFISI YA RAIS AFUNGUA SEMNA ZA WATALAAMU NA WAJASIRIAMALI WA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO MKOANI MWANZA.

George Yambeshi ambae ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa huduma za uchangiaji wa damu katika eneo la Pasiansi Mkoani Mwanza.

Serikali imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Mashirika na Taasisi binafsi zinazosaidia kutika kuboresha huduma mbalimbali ya kijamii, kwa ajili ya maendeleo wananchi hapa nchini.

Hayo yamesemwa Mkoani Mwanza na
George Yambeshi ambae ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma, wakati akizindua rasmi Semna za Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadiventist Wasabato Mkoani Mwanza jana Jumapili.
Yambesi alisema miongoni mwa mafanikio yanayoonekana Serikalini yanachangiwa na Taasisi mbalimbali kwa ushirikiano wa pamoja na Serikali, ambapo aliyataja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na Ujenzi na uendeshaji wa Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati ikiwa ni miongoni mwa mafanikio mengine mengi yanayochagizwa na Taasisi hizo hapa nchini.

Aidha aliongeza kuwa Serikali kupitia mpango wa ushirikishwaji wa Sekta binafsi, imeweka kipaumbele cha kushirikiana na Taasisi mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuleta maendeleo kwa jamii ya wananchi wa Watanzania, huku akiongeza kuwa nchi itaweza kupiga hatua kubwa na kwa haraka zaidi iwapo kama wadau wote wa maendeleo wa ndani watashirikiana na Serikali.
Katika hatua nyingine Yambesi alibainisha kwamba Serikali inakiri kwa dhati kuwa Taasisi za Kidini zimekuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na Serikali katika kuleta ustawi na maendeleo kwa jamii hususani katika huduma za Afya na Elimu.
                                                         
Kwa upande mwingine Yambesi aliwasihi Washiriki wa Kanisa la Waadventista Wasabato kuendelea na Moyo wao wa kujitolea katika huduma mbalimbali za kijamii, ambazo ni pamoja na huduma za Kiafya ambazo zimekuwa zikitolewa na Kanisa hilo.
Awali akisoma Risala mbele ya Mgeni Rasmi kwa niaba ya Kanisa la Waadventista Wasabato, Hobokela Mafwale alibainisha kuwa Kanisa hilo limekusudia kuendelea kutoa elimu inayochochea maendeleo na ustawi kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za Afya, Amani na Maadili kwa wananchi wote kwa ujumla ambapo aliongeza kuwa Kanisa hilo limekuwa likifanya kazi kwa mafanikio Makubwa kwa ushirikiana na Serikali ambapo limefanikiwa kujenga shule, vyuo, Vituo vya Afya sanjari na Hospitali.
Semna za Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mkoani Mwanza zilianza kutolewa tangu Septemba Nane na zinatarajiwa kufikia tamati Septemba 19 mwaka huu katika Hotel ya JB Belmont Jijini Mwanza.

Semna hizo zimeambatana na huduma mbalimbali za Kiafya ambapo wananchi wamepata fursa ya kupima Afya zao bure sanjari na zoezi la uchangiaji wa damu katika Maeneo ya Kanisa la Waadventista Wasabato lililopo Pasiansi na Buzuruga Mkoani Mwanza.
Wananchi waliojitokeza kupata huduma za Afya bure katika Katika Kanisa la Waadventista Wasabato lililopo Buzuruga Jijini Mwanza.
Wananchi waliojitokeza kupata huduma za Afya bure katika Katika Kanisa la Waadventista Wasabato lililopo Buzuruga Jijini Mwanza.
Vijana wa PathFinder kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato wakiimba Wimbo wa Taifa katika Ufunguzi wa Semna za Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa hilo Mkoani Mwanza zinazoendelea katika Ukumbi wa JB Belmont Hotel Jijini Mwanza. Semna hizo zinatarajiwa kufikia Tamati Septemba 19 mwaka huu.
Hobokela Mafwale (Kushoto) akisoma Risala ya Kanisa la Waadventista Wasabato katika ufunguzi rasmi wa Semna za Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa hilo.
 George Yambeshi ambae ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma akizungumza katika ufunguzi rasmi wa Semna za Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadiventist Wasabato Mkoani Mwanza
Mh.George Yambeshi ambae ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato baada ya kutembelea ujenzi wa Hospital ya Kanisa hilo iliyopo Pasiansi Mkoani Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.