MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MAOMBI YA PINGAMIZI LA KUSIMAMISHA BUNGE LA KATIBA.
Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam leo imetupilia mbali
maombi ya pingamizi la awali la kusimamisha Bunge la Katiba linaloendelea
mjini Dodoma, iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari Said Kubenea, kwa
kuwa wametumia kifungu cha sheria kisicho sahihi.
Kadhalika, mahakama hiyo imetupilia mbali
pingamizi
hilo la awali, kwa kuwa mlalamikaji ametumia kifungu cha sheria namba 2 kidogo cha (2) (JALA) ambacho hakina mamlaka ya kufungua maombi hayo mahakamani.
hilo la awali, kwa kuwa mlalamikaji ametumia kifungu cha sheria namba 2 kidogo cha (2) (JALA) ambacho hakina mamlaka ya kufungua maombi hayo mahakamani.
Uamuzi huo ulitolewa chini ya jopo lililoketi
la majaji watatu, wakiongozwa na Mwenyekiti Mh. Jaji Augustino Mwarija, Dr.
Fauz Twaib na Aloyisius Mujuluzi. Jopo hilo lilisema mahakama imetupilia mbali
pingamizi hilo la awali kwa sababu halina mashiko ya kisheria. Upande wa mlalamikiwa uliongozwa na Wakili wa
Serikali Mkuu, Gabriel Malata na mlalamikaji Peter Kibatala.
Awali, Mwanasehria Mkuu (AG) kupitia
Naibu Mwanasheria Mkuu, George Masaju kuiomba mahakama hiyo kutupilia mbali
pingamizi hilo kwa kuwa maombi yake ni batili kisheria na hayawezi
kuthibitishwa mahakamani, hivyo yatupiliwe mbali.
Katika pingamizi hilo lililoambatana na hati
ya kiapo, AG kupitia naibu wake, amedai kuwa maombi hayo ya mlalamikaji yana
dosari ambayo haiwezi kurekebishika kwa kuwa zinahitaji kifungu maalum cha
sheria kinachoipa nguvu mahakama ya kuridhia maombi hayo.
Mapema mahakamani hapo, Kubenea aliwasilisha
maombi ya pingamizi la awali ya kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa
usajili wa namba 29 ya mwaka 2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya
mamlaka ya Bunge yote yalifunguliwa mahakamani hapo jana chini ya Hati ya
Dharura.
Katika kesi ya msingi iliyopewa usajili
namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri
sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba chini ya vifungu vya 25 (1) na 25
(2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka 2011.
Pamoja na mambo mengine katika kesi hiyo ya
kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi
mahakamani hapo akiiomba mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo
ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri hiyo.
No comments: