LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERENGETI FIESTA 2014 MUSOMA KUFANYIKA LEO. MAPATO YATAKAYOPATIKANA KUWASAIDIA WAHANGA WA AJALI ILIYOTOKEA MKOANI MARA.

MKurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi, Bwa.Ruge Mutahaba (Wanne kulia) kwa niaba ya uongozi wa Clouds Media Group na PrimeTime Promotions  Ltd ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014, ametangaza rasmi kuwa onesho la tamasha hilo lililobeba ujumbe murua kabisa wa sambaza upendo, litafanyika leo jumapili ndani ya uwanja wa Karume Mjini Musoma Mkoani Mara.
Tamasha hilo la Fiesta
lilipangwa kufanyika juzi ijumaa mjini Musoma Mkoani Mara lakini kufuatia ajali mbaya iliyotokea katika kijiji cha Sabasaba, wilaya ya Butiama mkoani humo siku hiyo ya Ijumaa na kusababisho vifo vya watu zaidi ya 39 na wengine wengi wakijeruhiwa.
Ajali hiyo ilipelekea tamasha hilo kusitishwa ili kwenda sambamba na tukio zima katika kuwafariji wakazi wa Musoma na vitongoji vyake, kutoa mkono wa pole, ambapo Wasanii waliotarajiwa kushiriki tamasha hilo na Waandaaji walitoa msaada wa vifaa tiba kwa hatua za awali kusaidia majeruhi waliokuwa wakipelekwa hospitali ya rufaa mjini Musoma.
Pia imeelezwa kwamba katika shilingi 5,000 iliyopangwa kama kiingilio kwa ajili ya tamasha hilo la Serengeti Fiesta 2014 Musoma, Shilingi 2,000 itatolewa kwa ajili ya wahanga wa ajili iliyotokea Mkoani humo siku ya Ijumaa.

No comments:

Powered by Blogger.