LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAZAMA BALAA LA MADEE, IZZO BUSNESS NA SHAA KATIKA JUKWAA LA COKE STUDIO MWANZA.


Ilikuwa ni bonge moja la Burudani kutoka Kwa Wasanii wakali ambao ni Madee, Izzo Busness na Mwana dada Shaa ambae pia ni Mwakilishi wa kutoka Tanzania katika ile Show kubwa kabisa barani Afrika ya Coke Studio ambayo inawajumuisha Wasanii na Waandaaji wa Muziki kutoka Barani Afrika.   

Show hiyo inadhaminiwa na Kampuni ya Vinywaji ya Cocacola na katika kuwajali wateja wake, Kampuni hiyo imeamua
kuzunguka Mikoani na kutoa burudani kwa watumiaji wake wa vinywaji jamii ya Cocacola, burudani ambayo pia inaambatana na Promosheni ya Coke Studio ambayo humuwezesha Mtumiaji wa Kinywaji cha Cocacola kujishindia Muda wa Maongezi wa Dakika Tano, SMS na Vifurushi vya Internet.


Unachotakiwa kufanya ni kununua soda za Cocacola zenye vizibo vya rangi ya Njano na kisha kutuma nambari zilizopo katika vizibo kwenda namba 15441. Kumbuka kila soda ya Cocacola yenye kizibo cha njano ina zawadi. Hii ni kwa watumiaji wa Mtandao wa Vodacom pekee. Fuatilia kila Jumamosi saa tatu usiku Show ya Coke Studio kupitia TBC 1. Kwa mbaaali ni jengo la Kitega uchumi la Mwanza City Comprex, unaambiwa hiyo ni habari ya Mjini kwa nchi zote za Afrika Mashariki na Kati.
Madee akiperfom katika Jukwaa la Coke Studio. Ilikuwa noma maana hizo shangwe zake zilikuwa hatareee tupu.
Msanii Madee akitoa burudani hii leo katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza.
"Madee umebadilika, Yaa Sisomeki..."
"Nani kamwaga Coca yangu, Naulizaa" Hapana chezea Madee wewe.
Msanii Izzo Busness akiperfom katika Jukwaa la Coke Studio hii leo katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza.
Izzo Busness akimiliki Jukwaa la Coke Studio hii leo katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza. Hakika ilikuwa ni bonge la Show. Kwa mbaaali ni jengo la Kitega uchumi la Mwanza City Comprex, unaambiwa hiyo ni habari ya Mjini kwa nchi zote za Afrika Mashariki na Kati.
Mashabiki wakipata burudani katika Show ya Coke Studio iliyopigwa hii leo katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza. Show ya Coke Studio inadhaminiwa na Kampuni ya Vinywaji ya Cocacola ambapo kwa hivi sasa pia ukinunua kinywaji cha Cocacola chenye kizibo cha rangi ya njano unajipatia Muda wa Maongezi wa dakika tano, sms na vifurushi vya Internet. Unachotakiwa kufanya ni kutuma namba zilizoandikwa katika kizibo hicho kwenda nambari 15441 ili kujishindia zawadi hiyo. Kumbuka kila soda ya cocacola yenye kizibo cha njano ina zawadi.
Msanii Shaa (Katikati) ambae ni Miongoni mwa Wasanii wanaoiwakilisha Tanzania katika ile Show Kubwa kabisa ya Wasanii na waandaaji wa Mziki inayofahamika kama Coke Studio akiperfom katika Show ya Coke Studio leo katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza. Wengine ni Madencers wake.
Kiukweli Shaa amepiga bonge la Show akiwa na Madencers wake wawili katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza. Hii inadhihirisha kwamba Shaa alistahili kuungana na Wasanii wengine ambao ni Diamond Platnum na Lady Jaydee katika Kuiwakilisha Tanzania katika Show ya Coke Studio ambayo inawajumuisha Wasanii na Waandaaji mbalimbali wa Muziki kutoka barani Afrika ikiwa chini ya udhamini wa Kampuni ya Cocacola.
MC namba moja na MC namba mbili (Walioko pembeni) wakimnadi Moses Deogratius ambae ni Mshindi wa Kwanza wa Show ya Coke Studio (Katikati). Mshindi huyu ataungana na Washindi wengine Kutoka Mbeya, Moshi na Dar es salaam katika ile Show Kubwa kabisa ya Coke Studio inayorushwa kupitia kituo cha Runinga cha TBC 1 kila Jumamosi saa Tatu Usiku.
Amefahamika kwa jina la Moses Deogratius (Wa kwanza Kushoto) ambae ndie Msanii aliebuka kuwa Mshindi wa Kwanza kutoka Mkoani Mwanza na hivyo ataiwakilisha Mwanza kwa wale wasanii wa Mikoani nchini Tanzania katika ile Show Kubwa kabisa Barani Afrika inayodhaminiwa na Cocacola ambayo inafahamika kwa jina la Coke Studio ikiwa ni Msimu wa Pili. Tazama kila Jumamosi saa tatu Usiku kupitia TBC 1.
B 12 kutoka Clouds FM na Bon 2 Shine akiwa Jukwaani akiwandisha Madee, Izzo Busness na Shaa katika Sow ya Coke Studio iliyopigwa hii leo katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza.
B 12 Kutoka Clouds Fm ndie alikuwa Mc.
Mshikaji yuko Vizuri na alikuwa akiitendea haki hii Mashine. Show ya Coke Studio inadhaminiwa na Kampuni ya Vinywaji ya Cocacola ambapo kwa hivi sasa pia ukinunua kinywaji cha Cocacola chenye kizibo cha rangi ya njano unajipatia Muda wa Maongezi wa dakika tano, sms na vifurushi vya Internet. Unachotakiwa kufanya ni kutuma namba zilizoandikwa katika kizibo hicho kwenda nambari 15441 ili kujishindia zawadi hiyo. Kumbuka kila soda ya cocacola yenye kizibo cha njano ina zawadi. Shukurani za Dhati ziwaendelee pia NYANZA BOTTLING COMPANY ambao ni watengenezaji wa Vinywaji jamii ya Cocacola.

No comments:

Powered by Blogger.