UONGOZI CHADEMA WAKAMILIKA. HIKI NDICHO KIKOSI KAMILI.
Katika Uchaguzi uliofanyika juzi Jumapili ndani ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Mh. Freeman Aikael Mbowe
Alichaguliwa Tena kuwa mwenyekiti wa Chadema Taifa kwa kupata kura
789 sawa na asilimia 97.3 ya kura zote. Aliyeshinda nafasi ya Makamu mwenyekiti Bara ni Profesa Abdallah Safari kwa kupata kura 775 sawa a asillimia 95 na nafasi ya Makamu mwenyekiti Zanzibar alishinda Mh. Saidi Issa Mohamedi kwa kupata kura 645 sawa na asilimia 79.

Uchaguzi ndani ya chama
hicho cha CHADEMA umefikia tamati kwa kamati kuu ya chama
hicho kupata viongozi wake wa mwisho ambao ni Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu
Bara na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
|
Baada ya Uchaguzi wa Kumpata Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
Bara na Visiwani, uteuzi wa kuwapata viongozi wa nafasi zilizokuwa zimesalia
umekamilika. Walioteuliwa ni Dk.Willbrod Slaa ambae ametetea nafasi yake ya
Ukatibu Mkuu, John Mnyika ambae amerithi Mikoba ya Zitto Kabwe ya Naibu Katibu
Mkuu Bara na Salum Mwalim ambae amepata nafasi ya kuwa Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar. Viongozi
hao waliteuliwa na mwenyekiti wa chama hicho kama katiba inavyosema na hatimaye
baraza kuu likawapitisha wote bila kuwapinga.
Kutoka kushoto ni Naibu Mkuu zanzibar
Mh Salum Mwalimu Juma, Katikati ni Naibu katibu Mkuu Bara Mh John
Mnyika na Kulia ni Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa.

Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa.

Naibu Katibu Mkuu Bara Mh John Mnyika

Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mh Salum Mwalimu Juma
No comments: