LIVE STREAM ADS

Header Ads

HOSPITALI YA RAO MKOMBOZI KWA WATANZANIA WASIO NA UWEZO WA KWENDA KUTIBIWA NJE YA NCHI.

Lango la Kuingilia katika Hospitali ya Rao iliyopo Shirati Wilaya ya Rorya Mkoani Mara.
Hospitali ya Rao iliyopo katika Mji wa Shirati Wilaya ya Rorya Mkoani Mara imeelezwa kuwa mkombozi kwa Watanzania wasio na uwezo wa kugharamia gharama za Matibabu ya magonjwa mbalimbali ambayo mara nyingi matibabu yake yamekuwa yakipatikana katika Hospitali za Rufaa hapa nchini au wakati mwingine inje ya nchi.

Hayo yalibainishwa na baadhi ya Wananachi na Wagonjwa waliowahi kupata matibabu katika Hospitali hiyo walipokuwa wakizungumza na Mtandao huu kuhusiana na upatikanaji wa huduma za afya zinazotolewa katika Hospitali hiyo.

Miongozi mwa waliozungumza na mwandishi wa habari hizi Bi.Leah DM. Binagi ambae ni Mzazi wa Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa Radio Metro ya Jijini Mwanza sanjari na Blogger wa Mtandao huu George Binagi, alibainisha kuwa Hospitali ya Rao imekuwa Mkombozi mkubwa kwa Watanzania hususani wanaohitaji matibabu kwa njia ya Upasuaji kutokana na namna ambavyo imekuwa ikiwasaidia wagonjwa mbalimbali wanaofikishwa katika Hospitali hiyo kwa ajili ya Matibabu.

"Hospitali ya Rao kiukweli imekuwa Mkombozi kwa Watanzania mbalimbali hususani wanaohitaji matibabu kwa njia ya Upasuaji wengi wao wakiwa ni kutoka Mkoa. Awali wananchi walikuwa wakipelekwa katika Hospitali za Rufaa kwa ajili ya Upasuaji au hata wakati mwingine kutakiwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu, lakini kutokana na uwepo wa Hospitali hii wagonjwa wengi wamekuwa wakitibiwa hapa hapa Shirati na kuepuka usumbufu na gharama kubwa za kwenda kutafuta matibabu pahala pengine". Alieleza Bi.Leah ambae mwanae alifanyiwa upasuaji katika Hospitali hiyo na sasa anaendelea vyema.

Akiwa katika Hospitali hiyo, Mwandishi wa Habari hii alipata fursa ya kuzungumza na baadhi ya wagonjwa waliokuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali hiyo ya Rao, ambapo wagonjwa hao walibainisha kuwa kabla ya kufikishwa katika hospitali hiyo walikuwa wamezunguka katika hospitali nyingi bila mafanikio kutokana na magonjwa yaliyokuwa yakiwasibu ambayo yalikuwa yakihitaji upasuaji katika Hospitali za Rufaa lakini baada ya kufika katika hospitali hiyo walipatiwa matibabu na kueleza hali zao kuwa zinaendelea vyema.

Ufanisi na Ubora wa huduma unaolezwa kutolewa katika Hospitali hii ya Rao unaungwa mkono nami mwenyewe ambae ni mwandishi wa Habari hii (George Binagi) kwa kuwa nami ni mmoja wa wagonjwa ambao maisha yao yalinusurika baada ya kufikishwa hospitalini hapo na kupatiwa matibabu ambayo awali yalikuwa yakinipa mateso na manyanyaso makubwa katika maisha yangu.

HEKO HEKO DOKTA P.ZIKI MAKOYE KUTOKA HOSPITALI YA RAO ILIYOPO SHIRATI WILAYA YA RORYA MKOANI MARA AMBAE PIA NI MKURUGENZI WA RAO  HEALTH TRAINING CENTRE HUKO HUKO SHIRATI RORYA KWA NAMNA UNAVYOWASAIDIA WATANZANIA. LAKINI PIA HONGERA SANA WATUMISHI WOTE WA HOSPITALI YA RAO KWA UWAJIBIKAJI WENU.

Daktari P.Ziki Makoye MD, PhD kutoka Hospitali ya Rao iliyopo Shirati Wilayani Rorya, Pia ni Mkurugenzi wa Rao Health Training Centre kilichopo huko huko Shirati Wilayani Rorya Mkoa wa Mara.
Daktari P.Ziki Makoye MD, PhD kutoka Hospitali ya Rao (Kushoto) na Kulia ni Mmoja wa Wauguzi katika Hospitali hiyo.
Bi.Leah DM. Binagi ambae ni Mama Mzazi wa Mtangazaji/ Mwandishi wa Metro Fm na Blogger wa Mtandao huu George Binagi (Kushoto) akiwa katika Ofisi ya Daktari P.Ziki Makoye MD, PhD kutoka Hospitali ya Rao (alie katikati), pembeni ni mmoja wa wauguzi wa Hospitali ya Rao. 
Bi.Leah DM. Binagi ambae ni Mama Mzazi wa Mtangazaji/ Mwandishi wa Metro Fm na Blogger wa Mtandao huu George Binagi (Kulia) akiwa na Mmoja wa Wauguzi wa Hospitali ya Rao iliyopo Shirati, Rorya Mkoani Mara.
Na: George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.