LIVE STREAM ADS

Header Ads

UNAKARIBISHWA CHUO KIKUU CHA MZUMBE TAWI LA MWANZA.

Dr.Hawa Petro Tundui ambae ni Mkuu wa Skuli ya Biashara, Kampasi Kuu ya Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Ili kukabiliana na Ushindani katika soko la ajira katika nchi za Afrika Mashariki, Chuo Kikuu cha Mzumbe Tawi la Mwanza kimeandaa kozi fupi kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kiushindani wanafunzi wa vyuo vikuu sanjari na wafanyakazi wa makampuni na taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi.

Akizungumza na
Radio Metro Fm na Mtanzaniamedia Blog siku ya jana Jijini Mwanza, Dr.Hawa Petro Tundui ambae ni Mkuu wa Skuli ya Biashara, Kampasi Kuu ya Chuo hicho amezitaja baadhi ya Kozi fupi zitakazotelewa na Chuo hicho kuwa ni pamoja na Ugavi na Ununuzi (Smrt Supply chain Management; Current and Future trends), Kozi ya Kuendesha Miradi kwa njia ya Kisasa (Project Management and Evaluation using Computer Oeograms) sanjari na Kozi ya kuwajengea ifanisi wahudumu kuwahudumia wateja katika kiwango kinachokidhi ushindani uliopo (Customer Value Creation and Delivery).

Dr.Petro amebainisha kwamba Madhumuni ya Kozi hizo ni pamoja na kuwajengea uwezo wanafunzi na wafanyakazi wa Makampuni na Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi katika kukabiliana na ushindani wa ndani na ule wa nje.

Kuhusu ushiriki wa Kozi hiyo, Dr.Tunduri amebainisha kwamba watakaosoma watachangia gharama za uendeshaji ambazo ni Shilingi Laki nne na Elfu Tisini na Tano kwa wafanyakazi na Shilingi Laki Tatu kwa Wanafunzi wa Vyuoni huku akiongeza kuwa gharama hizo zinaweza kulipwa kupitia Mzumbe University Short Course anda Counsultancy, Account nambari 01J1076853301 iliyopo katika Benki ya CRDB.

Kwa wale watakaopenda kujiunga na Kozi hizo wanaweza kuzipata fomu za kujiunga ambazo zinapatikana katika Kituo cha Mzumbe kilichopo jengo la Eckaclif lililopo Isamilo Jijini Mwanza ambapo ofisi zao zipo ghorofa ya tatu au kupitia barua pepe ambayo ni ejchao@mzumbe.ac.tz.
MSIKILIZE HAPA DR.TUNDUI AKIFAFANUA ZAIDI.

Na:George Binagi-GB Pazzo.

No comments:

Powered by Blogger.