LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIBUDA ASEMA WANANCHI WA KANDA YA ZIWA NI MABWEGE NA MAKUBWA JINGA.

Mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi (CHADEMA) amewataka Wananchi wa Kanda ya Ziwa kubadilika na kuacha kuwa Makubwa Jinga na kuwa wa kwanza kupiga kelele ili Mawaziri wanaotoka Kanda ya Ziwa Kuvuliwa nyazifa zao za uongozi pindi wanapokumbwa na kashfa yoyote Serikalini.

Shibuda ameyasema hayo
leo wakati akizungumza na Wananchi kupitia Radio Metro kwenye Kipindi cha Pambazuko la Metro Fm kinachoruka kila Siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 06:00 hadi saa 09:00 za asubuhi.

Akiendelea kuzungumza Shibuda alienda mbali zaidi na kusema kuwa Wananchi wa Kanda ya Ziwa ni Mabwege kwa kuwa amekuwa akishangazwa na namba ambavyo wamekuwa wakichangia pakubwa katika kupiga makelele na hatimae Mawaziri wa Kanda ya Ziwa kuvuliwa nyazifa zao huku akibainisha kuwa kwa Kanda nyingine kama Kanda ya Kaskazini wananchi huwa hawana destruri ya kushabikia Viongozi wao wanaotoka Ukanda huo kuvuliwa nyazifa zao.

Miongoni mwa Mawaziri ambao wamewahi kupigiwa kelele kutoka Kanda ya Ziwa na hatimae kujivua ama kuvuliwa nyazifa zao ni pamoja na aliekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, aliekuwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja, Waliokuwa Mawaziri wa Wizara ya Mali Asili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Mh.Ezekiel Maige pamoja na aliekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema.

Wakitoa Maoni yao kuhusiana na alichokizungumza Shibuda, Wasikilizaji wa Metro Fm wameonekana kugawanyika katika Makundi mawili yenye nguvu sawa ambapo kundi la kwanza limeonekana kuunga Mkono kilichozungumzwa na Shibuda huku kundi la pili likionekana kukerwa na kauli za kiongozi huyo na hivyo kumwahidi Shibuda kwamba Mwaka huu katika Uchaguzi Mkuu atatambua kama kweli wao ni Mabwege na Makubwa jinga ama la!.

Katika hatua nyingine Mh.Shibuda amebainisha kwamba atagombgea nafasi ya Urais japo hakubainisha wazi kama atagombea nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Chama ambacho kwa hivi sasa wadadisi wa Siasa hapa nchini wanaeleza kuwa Misimamo mbalimbali ya Mh.Shibuda imekuwa ikiwaweka njia panda kama bado ana ushirikiano mzuri na viongozi wanaokiongoza chama hicho.
Na:George Binagi-GB Pazzo.

No comments:

Powered by Blogger.