LIVE STREAM ADS

Header Ads

PICHA ZA RAIS MUGABE AKILA MWELEKA ZAENDELEA KUTUMIKA VIBAYA.

Picha ikimuonyesha Rais wa Zimbabwe Mh.Robert Mugabe akila mweleka wakati akishuka katika ngazi mara tu baada ya kuwasili kutoka Ethiopia siku ya jumatano. Raisi Wa Zimbabwe aliwasili nchini humo na kutoa hotuba kwa wananchi waliofika kumpokea. Baada ya kuhutubia raisi huyo ambaye
anafikisha miaka 91 tarehe 21 mwezi huu wa pili (Februari) alianguka wakati akishuka katika ngazi kama ambavyo picha zinaonekana.
Picha Juu inaonyesha Rais Mugabe akijikwaa. 
Akiwa Ethiopia, Mugabe amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika (AU).
Hatimae Rais Mugabe akadondoka chini na kuwaacha wasaidizi wake wasijue cha kufanya.
Picha ambayo si halisi iliyotengenezwa baada ya Rais Mugambe Kuanguka.
Picha nyingine (si halisi) iliyotengenezwa ikimuonyesha Mugambo akitimua mbia na wanariadha.
Binagi Media Group tunachukua fursa hii kujadili nawe kwa pamoja, Je ni nani aliepiga picha za Rais Mugabe na hatimae kuzisambaza katika Mitandao ya Kijamii? Je sahihi picha za Rais kusambazwa baada ya tukio kama hili la Mugambe kuanguka chini?
Kwa Hisani ya Mtandao.

No comments:

Powered by Blogger.