 |
WASHIRIKI WA MDAHALO ULIOFANYIKA GOLD CREST HOTEL, MWANZA. |
Wagombea
katika nafasi mbalimbali za Kisiasa hapa nchini wameshauriwa kuwa makini na
ahadi wanazozitoa kwa Wananchi, kwa kuwa wao hawana uwezo wa Kutekeleza ahadi
hizo mbali na kuisimamia vyema Serikali katika kutekeleza majukumu yake.
Ushauri huo ulitolewa hii leo Jijini Mwanza katika Mdahalo wa
Tanzania Tuitakayo ulioratibiwa na Taasisi ya Mafunzo ya Biashara na
Mawasiliano Africa Mashariki EABMTI (East Africa Busness and Media Trainining
Institute) kwa Kushirikiana na Taasisi ya Twaweza ukiwa na lengo la Kuibua
vipaumbele vya Kimkoa vitakavyosaidia katika kuongoza Mijadala ya Kampeni za
Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika hapa nchini mwaka huu.
Akitoa Ushauri huo,
Robert Ng’winamila ambae ni Katibu wa Mbunge
wa Jimbo la Nyamagana (Chadema) alisema kuwa wapo baadhi ya wanasiasa hususani
wanaogombea nafasi za Udiwani na Ubunge wamekuwa wakitoa ahadi mbalimbali kwa
wapiga kura wao ikiwemo kuwajengea barabara wakati hawana uwezo wa kifedha wa
kuweza kutimiza ahadi hizo huku akidokeza kuwa wanasiasa (wabunge) wa aina hiyo
enzi za Mwalimu (Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere) alikuwa
akiwashusha majukwaani kwa kuwadanganya wananchi.
Ng’winamila aliwashauri wanasiasa wa aina hiyo kuacha kuwadanganya
wananchi na pindi wanapokuwa wakiongea na wananchi wawe wanaeleza wazi kwamba
wataishinikiza Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo barabara na
sio kuwadanganya kwamba wao ndio watakaoitekeleza miradi hiyo.
Wakati Chama cha Mapinduzi CCM kikichaka mdahalo huo, wawakilishi wengine
wa Vyama vya Siasa kutoka NCCR Mageuzi, Chadema na CUF walielezea baadhi ya
mambo wanayoyapa kipaumbele katika Jiji la Mwanza ambayo wamesema kuwa
wanaamini kama yatasimamiwa vyema Jiji la Mwanza litapiga hatua Kimaendeleo.
Meshack Micus Michael ambae ni Afisa wa Chadema Kanda ya Ziwa
Magharibi, pamoja na mambo mengine aliainisha kwamba Jiji la Mwanza linaweza
kujiendesha lenyewe kwa sababu linaweza kujisiamia kiuchumi ambapo ametolea
mfano uwepo wa Machinga zaidi ya elfu tatu waliopo Jijini Mwanza wakipangiwa
utaratibu mzuri na kulipa ushuru wa shilingi elfu thelathini kwa mwaka zinaweza
kupatikana shilingi milioni tisini na fedha hizo zikasaidia kutatua kero
mbalimbali ikiwemo upungufu wa madawati mashuleni, hilo likiwa ni eneo moja la
machinga miongoni mwa maeneo mengi.
Nae Hamza Shido ambae ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Jimbo la
Nyamagana CUF aliibua vipaumbele kadhaa vinavyopatikana Jijini Mwanza ambavyo
amesema kuwa vikitumiwa vyema vinaweza kusaidia katika kuleta maendeleo.
Shido alitolea mfano zaidi ya Shilingi Milioni 300 zinazotumiwa na
Halmashauri ya Jiji la Mwanza katika kusimamia zoezi la kuwahamisha machinga
katika maeneo yasiyo rasmi ambapo amesema kuwa fedha hizo zinaweza kutumika
katika kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi na hatimae kuchangia pato la Jiji
la Mwanza badala ya kutumika kuwalipa posho askari mgambo na askari polisi wanaoshiriki
zoezi la kuwaondoa machinga katika maeneo yasiyo rasmi.
Nao wadau mbalimbali walioshiriki katika Mdahalo huo waliomba
kuwepo kwa ufuatiliaji wa masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo mikakati ya
kufanya katika kuzuia mauaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na haki za watu
wenye ulemavu kwa ujumla katika kuelezea vipaumbele tofauti tofauti katika midahalo
ya kampeni za kuelekea katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu 2015 hapa nchini.
Kesho mdahalo kama huo utafanyika katika Wilaya ya Ilemela katika
Ukumbi wa Chuo cha VETA Nyakato ambapo Rosemary Mwakitwange ambae ni Mwenyekiti Mtendaji wa EABMTI
na muongoza midahalo hiyo, alibainisha kuwa midahalo hiyo imelenga kuibuka
vipaumbele vitakavyotumika katika kuongoza midahalo ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu
itakayokuwa ikiandaliwa na EABMTI na kurushwa katika runinga ya ITV. Kabla ya
Mwanza midahalo hiyo ilifanyika katika Mikoa ya Mbeya na Arusha.
 |
Wadau mbalimbali. |
 |
Wadau. |
 |
Wadau katika Mdahalo. |
 |
Washiriki wa Mkutano. |
 |
Washiriki wa Mdahalo. |
 |
Adam Ndokeji ambae ni Mratibu NGO's Kanda ya Ziwa. |
 |
Robert Ng’winamila (Mwenye Kinasa sauti) ambae ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (Chadema). |
 |
Hamza Shido ambae ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Jimbo la Nyamagana CUF (Mwenye Kinasa Sauti). |
 |
Mrisho Ntuga ambae ni Katibu NCCR Mageuzi Jimbo la Nyamagana (Mwenye Kinasa Sauti). |
 |
Aliesimama ni Meshack Micus Michael ambae ni Afisa wa Chadema Kanda ya Ziwa Magharibi. |
 |
Mshiriki akitoa Mawazo yake katika Mdahalo. |
 |
Mshiriki wa Mdahalo. |
 |
Wadau wakitoa Mawazo yao Katika Mdahalo. |
 |
Rosemary Mwakitwange ambae ni Mwenyekiti Mtendaji wa EABMTI na muongoza midahalo (Mwenye Kinasa Sauti) akiendelea kuongoza Mdahalo. |
 |
Rosemary Mwakitwange ambae ni Mwenyekiti Mtendaji wa EABMTI na muongoza midahalo. |
 |
Kushoto ni JeanPaul Fonkwa ambae ni Mwanasheria na Mshauri kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Biashara na Mawasiliano Africa Mashariki EABMTI (East Africa Busness and Media Trainining Institute), ambapo kulia ni Joel Maduka wa Kwa Neema Radio akinasa habari katika Mdahalo. |
 |
Kufahamiana na Salamu baada ya Mdahalo kumalizika zikaendelea. |
Na: George Binagi-GB Pazzo
No comments: