LIVE STREAM ADS

Header Ads

MULONGO AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA ALIEKUWA KOCHA WA TIMU YA TAIFA.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh.Magesa Mulongo akiuaga Mwili wa Aliekuwa Kocha wa Timu ya Taifa Sylvester Marsh.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh.Magesa Mulongo, jana ameongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa katika kuuaga mwili wa aliekuwa Kocha wa Timu ya Taifa na vilabu mbalimbali vya soka hapa nchini marehemu Sylvester Balunzi Mashishigulu Marsh.

Pia Viongozi mbalimbali wa Serikali, Siasa, Vyama vya Michezo, Wanamichezo, Wasanii pamoja na wananchi kwa ujumla walishiriki kumuaga Marehemu Marsh katika Uwanja wa Mirongon kabla ya kwenda kupumzishwa katika Makaburi ya Igoma Jijini Mwanza.

Marehemu Marsh alizaliwa Mwaka 1960 na alifariki dunia jumamosi iliyopita ya March 14 katika Hospitali ya Taifa Mhimbili Jijini Dar es salaam, alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu ya Saratani ya Koo yaliyokuwa yakimsumbua.
Picha na Gsengo

No comments:

Powered by Blogger.