LIVE STREAM ADS

Header Ads

AIKA NA NAHREEL WATUA JIJINI MWANZA KUDONDOSHA BONGE LA SHOW NDANI YA SAMAKI CARVIVAL.

Wasanii AIKA pamoja na NAHREEL tayari wako katika ardhi ya Rock City Mwanza-Mwanza kwa ajili ya Event kubwa kabisa inayotarajiwa kufanyika kesho April 11, 2015 katika viunga vya YUNGLONG CHINESE HOTEL JIJINI MWANZA ambayo inakwenda kwa jina la SAMAKI CARNIVAL.
Pichani kutoka Kushoto ni GB Pazzo, Aika, Bob White, Nahreel pamoja na Barry katika Studio za 99.4 Radio Metro Fm.
Picha na Jay Joh @Metro Fm & BINAGI MEDIA GROUP
Kazi ni moja tu hii, nayo ni kupata Samaki na maakuli ya aina mbalimbali yakisindikizwa na kilaji ukipendacho katika Viunga vya YUNG LONG HOTEL JIJINI MWANZA katika Event ya SAMAKI CARNIVAL msimu wa Tatu ambapo tayari AIKA na NAHREEL wako tayari kwa ajili ya kukupatia burudani murua kabisa. Kumbuka umateumate pale mlangoni wakubwa ni sh.10,000 na kinywaji mkononi huku watoto wakiingia kwa sh.5,000.
Kutakuwa na Michezo mbalimbali na time ni kuanzia saa 12:00 mchana na kuendelea.
Pichani kutoka kushoto ni Lulu Jama, GB Pazzo, 
Aika, Bob White, Nahreel pamoja na Barry katika Studio za 99.4 Radio Metro Fm
Na:FINE TOUCH EVENTS

No comments:

Powered by Blogger.